SI KWELI Picha hizi hazihusiani na maandamano ya Kenya ya Juni, 2024

SI KWELI Picha hizi hazihusiani na maandamano ya Kenya ya Juni, 2024

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Tangu Juni 18, 2024 nchi ya Kenya imetawala vyombo vya habari baada ya Wananchi wake kufanya maandamano wakipinga mswaada wa fedha (Soma hapa). Kufuatilia tukio hilo kumekuwa na picha mbalimbali zinasambaa mitandaoni na kuhusishwa na Maandamano ya Kenya ya Juni. Baadhi ya picha ni halisi na zinatokana na tukio hilo lakini nyingine zimezushwa na kuhusishwa na Maandamano ya Kenya. JamiiCheck itakusogezea baadhi ya picha zinazohusishwa na tukio hilo kimakosa.

1719208528114.png
 
Tunachokijua
Kuna picha inasambaa inamuonesha muandamanaji akipiga bomu kwa kutumia kifaa cha mchezo wa tenesi. Baadhi ya Kurasa za mitandao ya kijamii (tazama hapa) zimeijumuisha picha hiyo kama sehemu ya matukio layiyotokea katika Maandamano ya Kenya ya Juni, 2024. Tazama hapa chini:

1719210429527-png.3024324

Picha iliyowekwa na African_Archieves na kuhusishwa Maandamano ya Kenya ya Juni

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa picha hii iliyowekwa na @Africa_Archives haihusiani na Kenya na haihusiani na Maandamano ya Kenya ya Juni, 2024. Kupitia Google Reverse search inaonesha kuwa picha hii ilitumika mara ya kwanza Juni 3, 2016 (hapa) na ilielezea habari ya muandamanaji wa Ofaransa aliyekuwa akifanya kitendo hicho. Tazama picha chini

1719211191016-png.3024370

Picha ya Juni 3, 2016 ikimuonesha Muandamanaji wa Ufaransa.
Back
Top Bottom