<div class="bbWrapper"></div>
- Tunachokijua
- Kuna picha inasambaa inamuonesha muandamanaji akipiga bomu kwa kutumia kifaa cha mchezo wa tenesi. Baadhi ya Kurasa za mitandao ya kijamii (tazama hapa) zimeijumuisha picha hiyo kama sehemu ya matukio layiyotokea katika Maandamano ya Kenya ya Juni, 2024. Tazama hapa chini:
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa picha hii iliyowekwa na @Africa_Archives haihusiani na Kenya na haihusiani na Maandamano ya Kenya ya Juni, 2024. Kupitia Google Reverse search inaonesha kuwa picha hii ilitumika mara ya kwanza Juni 3, 2016 (hapa) na ilielezea habari ya muandamanaji wa Ofaransa aliyekuwa akifanya kitendo hicho. Tazama picha chini
Picha ya Juni 3, 2016 ikimuonesha Muandamanaji wa Ufaransa.