Mahamat Idriss Déby Itno Rais wa sasa wa Jamhuri ya Chad tangu aliposhinda uchaguzi wa rais mnamo Mei 2024. Alichukua uongozi wa nchi hiyo kwanza mnamo Aprili 2021 kama mkuu wa Baraza la Kijeshi la Mpito kufuatia kifo cha baba yake, aliyekuwa Rais Idriss Déby Itno
Madai
Kumekuwepo na chapisho kwenye mitandao ya kijamii linalodai kuwa wananchi nchini Chad wameandamana tena katika mji mkuu, N'Djamena, wakipinga uongozi wa Rais Mahamat Idriss Déby Itno, aliyeingia madarakani mwaka 2021 baada ya kifo cha baba yake, aliyekuwa Rais Idriss Déby Itno.
Chapisho hilo linadai kuwa maandamano hayo yalifanyika Jumapili, Novemba 1, na kwamba yanafuatia maandamano ya awali ya Oktoba 20, ambayo yalidaiwa kuvunjwa na vyombo vya usalama, huku baadhi ya waandamanaji wakiripotiwa kuuawa, kujeruhiwa na wengine kukamatwa.
Uhalisia
Hata hivyo, ufuatiliaji wa
picha kwa kutumia maneno muhimu umebaini kuwa picha zinazotumiwa kuunga mkono madai hayo si za tukio la hivi karibuni.
Picha hizo zinaonyesha waandamanaji wakitembea katika mitaa ya N'Djamena, Chad, wakiwa wamebeba bango lenye maneno ya Kifaransa
“Libérez les prisonniers politiques”, yakimaanisha
“Waachieni huru wafungwa wa kisiasa.”
Kwa mujibu wa taarifa zinazohusishwa na picha hizo, zilipigwa wakati wa maandamano dhidi ya utawala wa kijeshi nchini Chad mwaka 2021, baada ya jeshi kuchukua madaraka kufuatia kifo cha aliyekuwa rais Idriss Déby Itno.