Makamu Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Bara Mnamo Machi 25, 2025 aliwasili mkoani Njombe akitokea mkoani Mbeya mara baada ya uzinduzi wa Oparesheni ya chama hicho ya No Reforms, No Election, ambapo akiwa njiani Mbarali aliripotiwa kuzuiwa na polisi kufanya mkutano na wananchi.
Kumekuwapo na
picha zinasosambazwa mtandaoni zinazoonesha askari wa jeshi la polisi wakiwa na magari yenye rangi ya kijani zikihusishwa na tukio la kuzuiwa kwa mkutano wa John Heche Mbarali, Mbeya.
Uhalisia wa picha hizo
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa picha hizo zimepotoshwa kwa kuhaririwa kwa teknolojia ya Akili Mnemba kwa kuwekewa rangi ya kijani kutoka kwenye
picha halisi zilizochapishwa mtandaoni zikiwaonesha askari wa jeshi la polisi ambao walidaiwa kuzuia mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA
John Heche katika Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya.
Katika picha halisi gari za polisi zinaonekana kuwa na rangi nyeupe pamoja na namba za usajili PT 5356 na PT 5357 tofauti na picha zilizopotoshwa kwani namba za usajili hazisomeki, pia kukosewa kwa maandishi ya neno polisi upande wa pembeni wa gari.
Aidha sura za askari zinaonekana kutokuwa na uhalisia kwani sehemu za viungo zinaonekana kutokamilika mfano sehemu ya macho na mikono.
Hata hivyo kifaa cha utambuzi wa maudhui ya picha yaliyotengenezwa kwa Akili Mnemba kinabainisha kuwa picha hizo zimetengenezwa kwa teknolojia hiyo kwa
asilimia 99.