Picha: Hospitali ya Rufaa ya Chato iliyowekwa jiwe la msingi na Rais Filipe Nyusi. Kuhudumia takriban watu milioni 18 mikoa ya Kanda ya Ziwa

Kabla ya 2010 sikuwahi kusikia hili neno Chato. Siku hizi sidhani kama zinapita Siku mbili bila kulisoma mahali hili neno Chato...!
 
Mt Kilimanjaro...ni mlima mrefu kuliko yoote barani Afrika.
Wachaga wanaishi kwenye slopes za mlima huo..
KNCU kilikuwa chama chao cha ushirika.
 
Mkuu chato na yenyewe inajengwa iwe jiji kama Wuhan..kwa hiyo madaktari bingwa wasiwe na wasiwasi kuhusu kuendelea kula bata za jiji..
Kocha wa Simba mwenyewe kachomoa kukaa mbali na huduma za familia
 
Je haya yanafanyika kwa kujali populations ya watu walioko eneo hilo, Rais ajaye awe Majaliwa ili aiinue Kusini kusini kunastahili neema hii
 
"Unju Kuku wa Zebanga ,bin unuk Sese seko, (kwele) kutimba tu bukoba mji mzima tetemeko"

#Nikki Mbish (unjuneering)
 
Kati ya madhaifu makubwa katika uongozi wa Magufuli ni hili la kupendelea sana kijiji chake. Wakati akiwa waziri wa Ujenzi, alitumia madaraka yake ya uwaziri kuhamisha njia ya barabara fulani iliyokuwa inatoka Geita kwenda Bihalamuro ili ipitie Chato! Sasa haya ya kila kitu kizuri kujengwa Chato ni kukithiri. Sijapata data za kuonyesha kama ujenzi wa hospitali hii uliidhinishwa na bunge ingawa najua kuwa bunge letu huwa linapitishwa miswada bila kuisoma. Kuwa na hospitali ya rufaa Chato, wakati kuna nyingine pale Bugando ilhali mikoa ya kati hasa Tabora haina hospitali yoyote ya rufaa ni uendawazimu kabisa.
 

Ummy akiwa waziri wa afya alisema wamefanya feasibility study na ikaonekana Chato ndio eneo lililopo katikati ya mikoa ya kanda ya ziwa.

Akili kichwani hapo.
 

Na ruzuku ikiondolewa hapo Bugando Kanisa Katoliki litaimba haleluya bila kupenda.
 
Kwa mujibu wa wizara ya afya ni kwamba hospitali ya Rufaa ya Chato itahudumia takribani watu milioni 18....
Mbona nimesikia kuwa hata msumbiji watakuja Chato. Itabidi mkuu wa mkoa atoe na eneo la kujenga benki kuu maana Dar ni joto sana
 
Mambo mengine unaona kabisa ni ushauri mmbovu, huwezi kuweka epicentre ya matibabu mahala ambapo kuna population ndogo.

Geita mjini ndio jimbo lenye high density na population kubwa by far likiwa na watu laki nane; majimbo mengine yote hayavuki watu laki 3 katika mikoa ya Kagera, Kigoma, Shinyanga, Mara, Simiyu na Tabora.

Hospitali za rufaa zinajengwa kwenye miji mikubwa kwa sababu nyingi, moja wapo ni kuhakikisha inatumika at near full capacity ili kuondoa hasara, iwe inatoa easy access ya watu wengi, local amenities za ku support wafanyakazi na ndugu wa wagonjwa (vinginevyo 90% ya long stay patient ndugu zao watahitaji kutafuta guests house za kulala adding more cost to them) morale ya madokta na nurses kuwapeleka Chato which is pretty much a rural district.

Hakuna ubaya kujenga hospitali kubwa popote Tanzania (including Chato), lakini social-economic benefit factors za kufanya ivyo lazima zifikiliwe pia.

Hii hospitali itakuwa mzigo kwa serikali kuiendesha kwa miaka kadhaa mpaka Chato itakapokuwa.

Ukiwa raisi unaweza peleka chochote kwenu lakini uhalisia pia wa practicability ya hiyo investment lazima uzingatiwe kama waliotangulia walivyofanya.

Chato sio mahala pa kuweka hospitali ya rufaa sio kwa sababu raisi anatokea huko, la hasha epicentre ya kuweka hospitali kama hizo zina vigezo vyake na Chato as a rural district aikidhi.

It’s just a bad investment kama ilivyo kwenye kununua dreamliner na sasa cargo plane. Kuna wakati watu inabidi wamwambie ukweli ata kama wanaupenda uwaziri.
 
Watu ml 18 watatibiwa kwenye hiyo hospital.? Inabidi waiangalie Chato kwa jicho la pili. Na vipi kuhusu miundombinu huko Chato
 
Hakika lipo jambo nimejifuza kuhusu kupenda kwenu. Wapo watanzania wengi wanaishi mijini ambao hata makaburi ya babu zao hawayajui, wanasiasa ndio kabisa wanarudi nyumbani kipindi cha uchaguzi baada ya hapo wanasuburi mpaka mwaka mwingine was uchaguzi.

Wapo wasomi wengine wakirudi nyumbani wanafikia hotelini na ndugu wanakuja kumsalimia hapo, watoto zao ndo kabisa ni am fain, am guud, am okee. Chuki zisitufanye tusione nuru. Kuna kipindi tuliifahamu Marekani kuliko Bagamoyo.
 
700×365=18,000,000✓✓✓
Hahahahha
 
Mfyuuu. Mnatufanya watanzania watoto siyo!!!
 
Binafsi nafikiri na nashauri Serikali itoe idadi ya watumishi wanaohitajika hapo, halafu waajiriwe wapya wote. Ndipo uanze uhamisho wa kubadilishana na wazoefu/wakongwe. Lakini tukihamishia tu kutoka kwenye hoslitali zilizopo tutatengeneza upungufu mkubwa sana kwenye hospitali nyingine bila ulazima huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…