Mambo mengine unaona kabisa ni ushauri mmbovu, huwezi kuweka epicentre ya matibabu mahala ambapo kuna population ndogo.
Geita mjini ndio jimbo lenye high density na population kubwa by far likiwa na watu laki nane; majimbo mengine yote hayavuki watu laki 3 katika mikoa ya Kagera, Kigoma, Shinyanga, Mara, Simiyu na Tabora.
Hospitali za rufaa zinajengwa kwenye miji mikubwa kwa sababu nyingi, moja wapo ni kuhakikisha inatumika at near full capacity ili kuondoa hasara, iwe inatoa easy access ya watu wengi, local amenities za ku support wafanyakazi na ndugu wa wagonjwa (vinginevyo 90% ya long stay patient ndugu zao watahitaji kutafuta guests house za kulala adding more cost to them) morale ya madokta na nurses kuwapeleka Chato which is pretty much a rural district.
Hakuna ubaya kujenga hospitali kubwa popote Tanzania (including Chato), lakini social-economic benefit factors za kufanya ivyo lazima zifikiliwe pia.
Hii hospitali itakuwa mzigo kwa serikali kuiendesha kwa miaka kadhaa mpaka Chato itakapokuwa.
Ukiwa raisi unaweza peleka chochote kwenu lakini uhalisia pia wa practicability ya hiyo investment lazima uzingatiwe kama waliotangulia walivyofanya.
Chato sio mahala pa kuweka hospitali ya rufaa sio kwa sababu raisi anatokea huko, la hasha epicentre ya kuweka hospitali kama hizo zina vigezo vyake na Chato as a rural district aikidhi.
It’s just a bad investment kama ilivyo kwenye kununua dreamliner na sasa cargo plane. Kuna wakati watu inabidi wamwambie ukweli ata kama wanaupenda uwaziri.