Picha: Hospitali ya Rufaa ya Chato iliyowekwa jiwe la msingi na Rais Filipe Nyusi. Kuhudumia takriban watu milioni 18 mikoa ya Kanda ya Ziwa

Kwa nini marais waliopita hawakufanya mambo makubwa kama anayofanya Jpm?
Hawakuwa maraisi wa miundombinu tu, bali walikuwa maraisi wa sekta zote.

Pamoja na mapungufu yao, waliangalia sekta zingine na sio kuelekeza hela karibu zote kwenye miundombinu/ujenzi na ndio maana waliweza pia kuajiri, kuongeza mishahara, kusomesha wanafunzi wa vyuo vikuu kwa mapato yatokanayo na makato ya asilimia 8 tu na zingine kutoka serikalini, n.k.
 
Mkuu kila mji duniani ulikuwa mdogo na kutanuka
Naunga mkono
Hakika mkuu...

Itafika siku MAGUFULI atakumbukwa kwa wema mno...

Si Katika kipindi chake Cha UONGOZI....ila akiondoka....atakumbukwa zaidi ya WENGI WALIOPITA....

Mungu Mwenyezi atupe uhai mrefu aaamin pale tutakapoyahitaji sana maendeleo ya VITU NA WATU huku YAKISIMAMISHWA TU MAENDELEO YA WATU PEKEE.....

Muda utaongea.....
 
Halafu mwisho wa siku utakuta wengi wa manesi, madaktari, madaktari bingwa, wafamasia, wakuu wa vitengo nk. watakaohudumia hiyo hospitali ni kizazi kile kile kutoka kule kule Kaskazini mwa Tanzania (Kilimanjaro na Arusha). Alileta TRA Chato wale jamaa wa Kaskazini wakajaa ofisini, Akapeleka CRDB bado wale wale, akajenga Airport bado wale wale.

Wazee wa fursa wameshatinga chato, wanakwenda na upepo unapovuma, wanavuna pesa za wajinga wajinga Chato na kupeleka Moshi kuzitumbua kila Disemba!
 
Hawakuwa maraisi wa miundombinu tu, bali walikuwa maraisi wa sekta zote.
Sekta gani hizo Boss wangu? Kama ni elimu madarasa yamejengwa na walimu wanaajiriwa, afya ndiyo kama hivyo hospitali zimejengwa na madaktari wanaajiriwa, barabara, kilimo, mifugo,reli na hata ile iliyokufa ya dar tanga Arusha imefufuliwa,atcl ndege bwerere. Niendelee?
 
Hakika mkuu...

Itafika siku MAGUFULI atakumbukwa kwa wema mno...

Ninaamini hivyo mkuu,

Hatuwezi kuwa na miji michache ambapo watu wanajazana na kuzaliwa kila siku.

Tena kama angekuwa na mda zaidi natumaini angefanya mazuri zaidi.

Kwa kweli ana uthubutu na vision pia.

Huo mji ni wetu wote.

Hao wakuu wa mikoa wangekuwa na maono wangetafuta nao wawekezaji wa kuwekeza mikoani ili miji iendelee kukua na kuleta ajira kwa local people.

Ila jamaa anapambana
 
Ninaamini hivyo mkuu
Hatuwezi kuwa na miji michache ambapo watu wanajazana na kuzaliwa kila siku...
Swadakta.

Na hiki ndicho kipindi ambacho MADED na viongozi wao kutengeneza mazingira ya uwekezaji "aila" ya huo.

Wakidhamiria WATAWEZA.

Iko siku HISTORIA itamkumbuka JPM zaidi ya ilivyo sasa akiwa mamlakani.
 
Imepewa hadhi ya Hospital ya Kanda, sasa Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Musoma zipo nyanda ya juu kusini????

Uwepo wa hospitali ya kanda utachagiza ujenzi wa barababara nzuri, airport ndo kama hiyo... watu wa Bukoba na Kigoma watanufaika.

Kwa maoni yako ungependekeza ijengwe wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…