Picha: Hospitali ya Rufaa ya Chato iliyowekwa jiwe la msingi na Rais Filipe Nyusi. Kuhudumia takriban watu milioni 18 mikoa ya Kanda ya Ziwa

Picha: Hospitali ya Rufaa ya Chato iliyowekwa jiwe la msingi na Rais Filipe Nyusi. Kuhudumia takriban watu milioni 18 mikoa ya Kanda ya Ziwa

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ni kwamba hospitali ya Rufaa ya Chato itahudumia takribani watu milioni 18.

Kwamba wagonjwa 700 watahudumiwa kila siku.

Kwamba mikoa 6 ya kanda ya ziwa itahudumiwa na hospitali hii

Kwamba hospitali ya Rufaa Chato itahudumia takribani 1/3 ya Watanzania wote

Hivyo ni muhimu ujenzi wa hospitali hii ukakamilika mapema.

Maendeleo hayana vyama!
 
Jambo la msingi vifaa tiba viwepo vya kutosha, madawa, pamoja na madaktari bingwa wa kutibu hao wananchi, sio wagonjwa waende hapo halafu waandikiwe rufaa waende muhimbili, au wapangiwe tarehe nyingine ya kumuona daktari.

Muwakumbuke pia na wazee wetu wenye bima wasisumbuliwe wakifika hapo, watibiwe bila kutakiwa kulipia gharama zozote za ziada, na hata wale wasio na bima wapunguziwe gharama za matibabu yao, hili lifanyike kwa vitendo na sio kusema tu kwa maneno ya mdomoni.

Hospitali mpya lazima iwe na mambo mapya, kero zilizozoeleka miaka yote hazitakiwi kuwepo tena.
 
Halafu mwisho wa siku utakuta wengi wa manesi, madaktari, madaktari bingwa, wafamasia, wakuu wa vitengo nk. watakaohudumia hiyo hospitali ni kizazi kile kile kutoka kule kule Kaskazini mwa Tanzania (Kilimanjaro na Arusha)
Alileta TRA Chato wale jamaa wa Kaskazini wakajaa ofisini, Akapeleka CRDB bado wale wale, akajenga Airport bado wale wale......

Wazee wa fursa wameshatinga chato, wanakwenda na upepo unapovuma, wanavuna pesa za wajinga wajinga Chato na kupeleka Moshi kuzitumbua kila Disemba!

Acha ukabila na ukanda, kama unaamini hivyo basi jikite zaidi huko visiwani.
 
Hakika ni hatua kubwa mno ITAKAYOPIGWA.

Kuhudumia wananchi milioni 18 wa nchi hii si jambo DOGO haswaaa.

Tunategemea mengi yatafanywa na kuachwa kama LEGACY kwa ajili yetu wananchi kipindi hiki cha awamu ya 5.
 
Back
Top Bottom