Picha: Huu ndio "MGAHAWA" mpya wa Ray C

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Kupitia Instagram ya Ray C ameandika: Taasisi ya Ray C Foundation iliyo chini ya muimbaji mkongwe, Ray C imefanikiwa kuongeza mradi mpya wa mgahawa ambao utatoa fursa ya ajira kwa vijana waliojikomboa kutoka kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Matunda ya Ray C Foundation, Namshukuru Mungu kwa kuendelea kutubariki , kupitia foundation yetu tumeanza kufungua miradi mbalimbali ili kuwawezesha vijana walioamua kubadilika na kuachana na dawa za kulevya kupata ajira ili waweze kuendesha maisha.

Kwa kuanza Ray C FOUNDATION imefungua mgahawa nje ya hospitali ya Mwananyamala ili kuwawezesha wagonjwa na wauguzi waweze kupata chakula cha kila aina na kitamu,mgahawa Wetu una chakula cha kila aina na tunachukua oda za harusi, kitchen party msiba, birthday, mikutano nk.

Menu yetu pilau Kuku ,wali Kuku ,wali nyama, pilau Kuku, pilau Samaki, ugali Samaki, tambi na nyama ya kusaga, macaroni, beef burger, Shawarma, sambusa ,Bagia za kunde ,chapati ,ugali wa muogo, kisamvu,bamia , mlenda,nyama chomaa, mbuzi choma , ndizi choma ,urojo, ndizi bukoba / mshale,vitumbua ,juice ya miwa ,juice ya karoti, tikiti ,juice ya avocado, .juice ya ukwaju, juice ya mango !!!chocolate cake,cake ya zabibu kavu ,chapati za maji etc agiza chochote utaletewa hadi mlangoni pia tunafanya delivery nyumbani , maofisini na mikutanoni.
 

Attachments

  • 1411246145421.jpg
    36.6 KB · Views: 4,364
Mmh!! Hongera zake kajitahidi, ila mmh kwa kweli hapana unafki mbaya, huu ndo mgahawa kweli wa kumiliki staa kama yeye? Na hao akina mama mwantumu uko tandale wamiliki nini? Tatizo hawa mastaa wanajisahau mno na huo uwe mfano kwa mastaa wote, mwenzie jide yupo mbali ye anahangaika na migahawa ya walevi.
 
ray c kariakoo alikuwa na mtaa huyu ...maduka yake, nymba ndio kwishneyanaanza upya. dahhh nampenda huyu dada najisikia vibaya sana kuona anaanza upya
 
Dinazarde naona umbea mtamu mpaka umesinzia, aya usiku mwema, kesho saa kumi na mbili kazini kama kawa
 
Last edited by a moderator:
Kiukweli Ray C amebadilika sana ......Kama kuna binti superstar anataka kujifunza kitu amtafute .....mimi ni moja ya watu tuliomshawishi aanze kujiita DJ Ray C baada ya kuridhishwa na uwezo wake hasa kupitia kipindi chake enzi hizo cha music Box kupitia EA radio kila jmosi.Ray C binafsi nakufatilia na kukutakia maisha ya mfano kwa jamii yetu......hongera sana ......
 

Acha wivu! Unaposema mgahawa wa walevi unamaanisha walevi hawana hela!?
Kwa jide kuna nini cha maana pale,mbona wanajaa watu wa vipato vyote!
 

Ray c anaanza upya....from teja hadi kufikia hapo Mimi ninaona amejitahidi sana . Mungu amsaidie apande tena km zamani
 
Kwa hali ya ualosto alokuwa nayo hii hatua ni ya kumpongeza, anaonesha yupo determined. Ukweli ni kwamba ameanzia chini sana japo sio jambo baya maana ndo hali halisi inayomkabili. Lakini, anatakiwa aendeshe huu mgahawa kibiashara sio kama hisani kwa waliokuwa drug addicts. Hili ni kosa ambalo naona anakaribia kulifanya. Afuate principles za biashara ili ajenge image ya mgahawa wake kibiashara. Lengo kuu linapaswa kuwa mgahawa ujiendeshe kwa faida na suala la kutoa ajira liwe ni ziada tu.
 
Acha wivu! Unaposema mgahawa wa walevi unamaanisha walevi hawana hela!?
Kwa jide kuna nini cha maana pale,mbona wanajaa watu wa vipato vyote!

Usilinganishe uchafu ule na mgahawa wa jide wewe, acha unafki, hata mastaa wenzie sidhan kama wataenda pale, pako local sana na ni tofauti na level yake ya kistaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…