Picha: Huu ni uchekeshaji ama udhalilishaji?

Kuiga sauti za makabia fulani kuwa ni washamba huo ndio udhalilishaji. Ila kuvaa malapulapu ni kukosa ubunifu hakuna aliyedhalilishwa hapo.
 
Tatizo kubwa la wachekeshaji wa kwetu ni elimu ya hicho wanachofanya kuachana na vipaji walivyonavyo. Wengi wanajikuta wanavuka mipaka ya uchekeshaji mpaka kujikuta wanadhalilisha watu wa makundi flani ktk jamii mfano kundi la walemavu wa viungo, watu wa kabila flani, watu wanaofanya kazi ya aina flani ktk kujipatia ridhiki na n.k
 
Jamani hii ni tanzania sio ulaya, msipende kufananisha wachekeshaji wa mbele uko na bongo huku kibongo bongo lazima uangalie namna gani ya kufanya komedi hili upate ugal sasa embu angalia na jamii ya ulaya ilivyo na jamii yetu ya kibongo bongo, tusiwe wepesi sana wa kukosoa embu tuangalie na namna ya kubadilisha hizo komedi zetu
 
Kwani hawezi chekesha akivaa tu vizuri, huyu jamaa mda mwingine anakosa content kabisa
 
Baadhi wanadhani uchekeshaji unaendana na kuvaa nguo kubwa, kuongea kwa lafudhi ya jamii Fulani na mengineyo ila sikatai inaweza kuwa sawa ila unaweza ukavaa vizuri tu ukaenda kwa stage ukaonesha kipaji chako na watu wakakiona.
Kila comedian ana aina yake ya uchekeshaji, usitake kila mtu awe kama fulani. Huo ni uzwazwa.
 
Bongo hakuna vipaji...vipaji halisi vya utotoni wazazi wanavipuuzia...matokeo yake watu wanaibuka na vipaji vya ukubwani..vinavyotokana na kupigwa na maisha.
 
Kila tukio na mahali pake.
Ukienda sehemu ya mataputapu nyama choma ni vichwa vya kuku, utumbo, na maiguu yake. Na bei zanaanzia jero.
Ukienda baa za Temeke myamachoma bei yake inaanzia buku.
Ukienda baa ya Hoteli ya Holiday Inn, nyama choma bei yake inaanzia 50,000/=
Sasa uchaguzi ni mtu binafsi akajirushe wapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…