Rais Samia azidi kuweka records:
Mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa JMT.
Rais wa kwanza kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la chama cha upinzani.
Rais wa kwanza kukubalika na watanzania wa makundi mengi ikiwemo vyama vya upinzani.
Rais wa pili (wa kwanza ni Ali Hassan Mwinyi) baada ya kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi vya upinzani kutochafua mikono yake kwa damu za wanachama au wapenzi wa vyama vya upinzani: Ikumbukwe wakati wa utawala wa Mkapa, wanachama wa CUF zaidi ya 20 waliuawa na jeshi la Polisi. Wakati wa Kikwete, kuna wanachama wa CHADEMA waliuawa kwa bomu kwenye mkutano Arusha, mwenyekiti wa CHADEMA Arusha aliuawa kwa chainsew machine kwa kukatwa kichwa, Mwenyekiti wa CHADEMA wa mkoa wa Geita aliuawa kwa kukatwa mapanga na kundi linaloaminika kufadhiliwa na Musukuma; wakati wa Magufuli ilikuwa kilele cha uovu wote dhidi ya wapinzani.