PreGE2025 POTOSHI Picha ikionesha nyomi ya watu kwenye Operesheni ya 'No reforms No election' Mei 14, 2025

PreGE2025 POTOSHI Picha ikionesha nyomi ya watu kwenye Operesheni ya 'No reforms No election' Mei 14, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu hizi picha ni za mwaka huu?

1747381214894.jpeg

1747290871020.png
 
Tunachokijua
Madai

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwapo na picha inayosambaa inayowaonesha wanaonekana kuwa ni wafuasi wa CHADEMA wakiwa wamekusanyika kwa wingi, ikiambatana na madai kuwa picha hiyo ni ya kutoka kwenye moja ya mikutano ya kampeni ya ‘No reofrms No election’. Tazama hapa na hapa

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia picha hizo na kubaini kuwa mojawapo ya picha hizo si ya mwaka huu. Ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo ya Google reverse image umebainisha kuwa picha hiyo si ya mwaka huu bali ni ya mwaka 2015.

Ufuatiliaji umebaini kuwa picha hiyo ni ya Oktoba 9, 2015 kwenye moja ya mikutano ya kampeni ya Urais mwaka 2015 ambapo Edward Lowassa ndiye aliyekuwa mgombea kupitia CHADEMA kwa mwamvuli wa UKAWA.

Tovuti ya Samdach Oktoba 10, 2015 ilichapisha taarifa yenye kichwa “Mafuriko ya Lowassa huko Moshi, Karatu na Siha jana Oktoba 9”, ndani waliandika kuhusu matukio yote yaliyotokea katika mkutano huo huku miongoni mwa picha zilizoambatanishwa ni hiyo iliyosambazwa tena kwenye mitandao ya kijamii Mei 14, 2025 ikidaiwa kuwa ni ya kwenye mkutano wa “No reforms No election’.

Tovuti mbalimbali pia ikiwemo Zanzi news online na Muungwana blog zilichapisha taarifa hiyo kwa nyakati tofauti kati ya Oktoba 9 na Oktoba 10, 2015 kuhusu mkutano huo na miongoni mwa picha walizoziambatanisha ni hiyo inayosambazwa mwaka 2025.
Back
Top Bottom