Sasa Depay na Samata wanacheza namba moja? Hata hivyo ni miezi mi 4 tu nyuma huyu Depay alifanya makubwa katika World cup na pia alikuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uholanzi. Tunapenda ushabiki bila kuangalia facts na ndio maana tulimpanikisha Mkwasa na akafanya subs zisizo na mpango.
Back to topic; Kawaulize wachezaji wakubwa waliowahi kufundishwa na LVG watakuambia jamaa ana mfumo mgumu sana. Jamaa yuko hard sana,anapenda kutumia viungo wengi wa kukaba na ndio sababu ya Depay kushindwa kufit, siyo yeye tu hata Rooney anapata taabu. Ilimtokea Di Maria last season ... Hawapi wachezaji uhuru bali anataka wastick kwenye mfumo. Fergie yeye alikuwa dynamic, ndio maana aliweza kuchukua kombe hata kwa kutumia wachezaji wa kawaida sana.
Ukitaka kujua LVG ni mkorofi muulize Luca Toni alipokuwa pale Baryen Munich. Msimu wa nyuma Luca Toni alimaliza na magoli 40+ lakini LVG alipongia jamaa hakufikisha hata goli 20.
Kwa level EA Samata anajitahidi, tatizo ni kuwa hataweza kucheza ligi kubwa dunianni kwa sbb ya nafasi ya Tz kwenye viwango vya Fifa. Labda ajaribu Ubelgiji, au Urusi, au Denmark, akibahatika sn France. Kwa EPL au La Liga ni lazima utoke katika nchi iliyo ndani ya 70 bora. Ngoja nikomee hapo!