upupu255
JF-Expert Member
- Sep 4, 2024
- 418
- 550
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 64 raia wa China alidungwa na nondo ya chuma baada ya kuanguka juu yake kutoka urefu wa takribani futi sita.
Wenzake kazini walisema aliteleza alipokuwa akifanya kazi juu ya jukwaa. Mwanaume huyo kutoka Chenzhou, katika Mkoa wa Hunan katikati mwa China, alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji wa dharura katika Hospitali ya First People’s Hospital.
Daktari Zhang Jianwen alisema kuwa takribani inchi 24 ya nondo ya chuma sawa na robo tatu ya urefu wake wote iliingia mwilini mwa mwanaume huyo kupitia makalio yake. Nondo hiyo ilipenya kwa kina hadi ndani ya kifua chake, lakini kwa kushangaza aliendelea kuishi. Hospitali ilieleza kuwa mwanaume huyo alipata majeraha katika viungo vingi vya ndani, ikiwemo moja ya mapafu yake, kutokana na ajali hiyo.