KWELI Picha inayodaiwa kuwa ni ya tukio la moto huko Nebraska Imetengenezwa kwa Akili Unde

KWELI Picha inayodaiwa kuwa ni ya tukio la moto huko Nebraska Imetengenezwa kwa Akili Unde

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
1774334209592.png
 
Tunachokijua
Picha inayoonesha tukio la moto imesambazwa sana mtandaoni na kudai kuwa picha hiyo ni moto unaoendelea Nebraska Mwezi Machi katika jimbo hilo.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia nyenzo za kidigitali umebaini kuwa hakuna chanzo cha kuaminika au mamlaka rasmi iliyochapisha picha hii sambamba na taarifa za moto.

Kwa mujibu wa ripoti ya AFP inayomnukuu Chad Bladow, meneja wa mpango wa moto wa shirika la The Nature Conservancy huko Nebraska, alisema kuwa ishara kuu kwamba picha hiyo si ya kweli ni kwamba barabara za lami kwa kawaida hazishiki moto.

Katika barua pepe ya mnamo Machi 19, alisema kuwa mandhari ya picha hiyo pia hayakuendana na maeneo ya moto mkubwa minne ya nyikani iliyokuwa ikiathiri Nebraska, jambo ambalo lilithibitisha zaidi kuwa picha hiyo ni ya kutengenezwa.

Mashamba kwenye picha hiyo ni madogo na ya mraba, wakati Bladow alisema kuwa maeneo ya Morrill na Cottonwood kanda mbili kuu za moto zilizodumu kwa muda mrefu zaidi huko Nebraska hutumia mifumo ya umwagiliaji ya center pivot (mduara) na "ikiwa picha hiyo ingekuwa imepigwa kutoka kwenye mojawapo ya moto hiyo miwili, tungepaswa kuona mashamba ya duara."

Pia alihoji rangi ya moshi. "Pangefaa kuwa na moshi mweupe zaidi, lakini picha inaonyesha moshi mweusi pekee."

Aidha nyenzo za kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa Akili Unde zinabainisha kuwa uwezekano wa picha hiyo kutengenezwa kwa teknolojia ya AI ni zaidi ya asilimia 99.​

1774720512234-png.3563863
AI imetumika kugenerate hii picha kuonyesha kua ni wild fire huko Nebraska
 
Video hii imetengenezwa kwa kutumia Akili Unde ikirejelea matukio ya moto ambayo yalikuwa yanaendelea kuwaka katika Eneo la Nebraska kutoka Nchini Marekani
 
Rangi ya moshi lakini pia moto unawezaje kukatiza kwenye lami na kuhamia eneo la pili?
 
Back
Top Bottom