sunshine1
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 539
- 291
Sometimes kumbe huwa una point. Sasa ongea basi na hao wenye kijani aka kikundi cha dhaifu wafanyie kazi mawazo yako. Maana wewe ni mshabiki wao mkubwa maybe watakusikiliza!
Hapo wenye zoo wanamakosa na watu wazima waliokwenda na huyo mtoto zoo wana makosa, hiyo hadithi ya kwenda chooni na mwingine kufatwa Inchon haina mshiko wala ukweli ndani yake. Wote (wenye zoo) na waangalizi wa huyo mtoto walikuwa wazembe.
Hapa Serikali lazima iingilie kati, hawa wenye ma zoo wana utaalam wa hizi zoo au wanapewa tu vibali kiushikaji? faida ya hiyo zoo kwa taifa ni nini au kwenda kuwatesa tu wanyama?
Kama ni mimi Tanzania ingeweka zoo ya wale wanyama adimu tu na hiyo zoo iwe inafanyia kazi kuwaongeza idadi yao na sio kwa ajili ya kuwafungia tu kuwacha watu wakatazame. Wange promote hawa watoto wawekewe huduma za kuwapeleka mbuga za wanyama wakajionee live. Faida inayopatikana kutoka kwa watalii wanaokuja kutazama hawa wanyama ingemegwa na kuanzisha idara ambayo itakuwa inawachukuwa mashuleni na kuwapeleka mbuga za wanyama hawa watoto zetu. Inawezekana, ni mipango tu.