Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Nyaraka nyingi na picha za historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika zipo mikononi mwa watu binafsi.
Nimepata picha kutoka kwa watoto wa akina Dossa Aziz, Sheikh Abdallah Chaurembo, wanafunzi wa Sheikh Hassan bin Ameir, wajukuu wa Jumbe Tambaza, watoto wa Ali Msham, watoto wa Abdallah na Maulidi Kivuruga wa Tabora, watoto wa Yusuph Chembera na Salum Mpunga wa Lindi, watoto wa Yusuf Olotu wa Moshi, watoto wa Sadik Patwa wa Tanga, wajukuu wa Makata Mwinyi Mtwana wa Tanga na watoto wa Sheikh Abdallah Rashid Sembe wa Tanga, nimepokea picha kutoka kwa wajukuu wa Affande Plantan, kutoka kwa Mzee Kissinger, Jim Bailey (Africa Collection, Johannesburg) kwa kweli wachangiaji picha ni wengi na hapa nitaeleza kuhusu mchango wa sisi wajukuu wa Salum Abdallah.
Nimepokea picha za babu yangu Salum Abdallah kutoka kwa binamu yangu Bi. Mgeni bint Farijallah kutoka Tabora picha ambazo alizihifadhi baba yake na baada ya kifo cha baba yake mama yake akawanazo.
Picha hizi zilihifadhiwa baada ya kifo cha babu mwaka wa 1974 na kwa miaka 45 hakuna aliyekuwa anajua zilipo kiasi cha kuamini kuwa zimepotea.
Picha hizi ni katika historia ya siasa za vyama vya wafanyakazi Tanganyika wakati wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) iliyoundwa mwaka wa 1955.
Baada ya kuhangaika sana kuzitafuta watoto wa Kassanga Tumbo aliyekuwa Katibu muasisi wa TRAU babu yangu akiwa Rais muasisi waliniletea picha kutoka Sikonge lakini zilikuwa zimharibika sana kwa kukosa matunzo ndipo nilipotembelewa na Bi. Mgeni na nikamuuliza kuhusu picha.
Jibu lake lilikuwa nitazitafuta kwa mama.
Hakichukua muda akaniletea picha nzuri kabisa zenye ubora.
Picha nyingi nimepata katika Maktaba ya Sykes na sababu kubwa ni kuwa wao wamekuwa katika harakati hizi kutoka mwaka wa 1929 na vitu vingi walivihifadhi katika nyumba zao.
Hata hivyo zipo baadhi ya picha nimepata kwa watoto wa wazalendo wengine na nyingine kwa watu wa kawaida na mpaka hivi sasa bado napokea picha.
Viongozi wa TRAU
Mstari wa kati kulia ni Salum Abdallah akifuatiwa na Kassanga Tumbo. Sijaweza bado kupata majina ya hao wengine.