GE2025 PICHA: Kwa Hakika Rais Samia Ni Chaguo La Mungu Kwa Haya Mafuriko Ya Wana Arusha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Watanzania,

Haihitaji Elimu ya Dini kulitambua hili, haihitaji uoteshwe ndoto kulifahamu hili. Kwa hakika Pasipo shaka wala wasiwasi wala kigugumizi wala simile wala hofu ni dhahiri na wazi kabisa kwa ishara zote ya kuwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Shujaa wa Afrika na nuru ya wanyonge ni Chaguo la Mungu Mwenyewe na aliyeinuliwa kwa Mkono wa Mungu Mwenyewe.

Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe kuliongoza Taifa letu. Ni yeye ndiye aliyempatia kibali mbele ya watanzania,ni yeye Mungu Mwenyewe ndiye aliyembele na popote awapo Mama yetu. Kwa hakika Rais Samia ameiteka mioyo ya watu.

Kwa kilichotokea Arusha, kwa mapokezi haya, kwa mafuriko ya watu ,kwa shangwe la wananchi,kwa furaha walioonyesha wana Arusha kwa Mama yetu Mpendwa ni wazi kuwa Mama ni Mtu wa Watu ,kiongozi wa watu mwenye kuaminika ,kupendwa na kukubalika.

Unajua kwanini imekuwa hivyo mpaka Kwa wana Arusha Kumpokea Rais wetu Mpendwa kwa kishindo? Jibu ni kuwa Mama Amegusa Maisha ya wana Arusha ,Hakuna aliyeachwa nyuma ,hakuna ambaye hajafikiwa na mkono wa Mama,hakuna ambaye hajaona matunda ya jasho lake,hakuna aliyeulizwa na Mama kimaamuzi au kisera au kisheria.

Kila Mwaka Arusha ameshuhudia namna secta ya utalii ilivyofanya vizuri awamu hii na kuzalisha ajira na fursa mbalimbali kwa vijana na makundi mbalimbali kuanzia Mama ntilie , bodaboda, Bajaji,waongoza watalii,wamiliki wa mahoteli na magari ya kusafirisha watalii ,machinga na wafanyabishara mbalimbali na wa biashara tofautitofauti wameona namna hali ilivyokuwa nzuri na kuongeza kipato chao awamu hii ya Mama yetu msikivu na mwenye upendo kwa watu wote.

Wana Arusha wafanyabiashara wameona biashara zao zikistawi ,kukua na kushamiri wakati huu wa Mama kuliko wakati mwingine wowote ule katika historia ya Taifa letu. Wafugaji nao pia wameona namna ambavyo secta yao ikikua na kuwaletea maendeleo. Ndio sababu ya leo hii watu kufurika na kumiminika kumlaki ,kumpokea na kumsikiliza Rais wetu Mpendwa kwa Bashasha,furaha na shangwe kubwa lililolindima na kuitetemesha kanda ya kaskazini nzima.
Screenshot_20251002-155725_1.jpg

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Masikini nimeona wafanyakazi wa Ato z wakilalamika kusombwa kwa nguvu kwenda kujaza uwanja, yaani kwa lazima upende usipende, wao tu ni zaidi ya watu elfu tano, kama unabisha kawaulizr, nimesikitika sana, nimeona wakishushwa kwenye mabasi yao yapatayo 20 hivi, wanamwagwa kisha mabasi yanarudi kusomba wengine.
 
Nashangaa ujasiri gani aliyonao wa kuendelea na kampeni
 
Kwani ni rais gani wa nchi hapa Tanzania ambaye hakuwahi kuwa mpango wa Mungu na hakuwa kipenzi cha watu?
 
Kumbe huyo mama aliyewafikia mamilioni ya watanzania ndio kwa kuwapa maji taka katika mabomba ya maji safi??

Kwa mtindo huu tofauti ya UCHAWA na UMALAYA siioni.
 
Ukiachilia mbinu ya upigaji picha katika angle ili kuonyesha watu wamejaa, na software editing ya hio picha..(tuliofanya graphics tunaelewa hili.)

Hapo kuna watumishi wa serikali karibu Arusha yote..(Hawa imewalazimu kwenda ili kulinda vibarua vyao kuhofia kupoteza.)

Kuna wanafunzi wa secondary..

Kuna migambo na wanajeshi waliolazimishwa kwenda hapo..

Kuna wananchi waliokwenda kuangalia wasanii..(hawa wamekwenda kwa hiari).

Kuna wale wananchi waliohongwa pesa, chakula au nguo kufika hapo..

Asilimia 5-10 tu ya wananchi hapo ndio wamekwenda kwa hiari yao, hao waliobaki asilimia 90-95 wamehongwa wengine kulazimishwa ili kulinda vibarua vyao...

Samia hakubaliki , huo ni ukweli mchungu.

Hapo anahonga mabilioni ya pesa, hivi anashindana na nani? mbona watu wameshamuachia ashindane peke yake? atulie tu nyumbani siku ya uchaguzi hana mpinzani.. ya nini kufanya maigizo.. 😂 😂
 
Ndugu zangu Watanzania,

Haihitaji Elimu ya Dini kulitambua hili, haihitaji uoteshwe ndoto kulifahamu hili. Kwa hakika Pasipo shaka wala wasiwasi wala kigugumizi wala simile wala hofu ni dhahiri na wazi kabisa kwa ishara zote ya kuwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Shujaa wa Afrika na nuru ya wanyonge ni Chaguo la Mungu Mwenyewe na aliyeinuliwa kwa Mkono wa Mungu Mwenyewe.

Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe kuliongoza Taifa letu. Ni yeye ndiye aliyempatia kibali mbele ya watanzania,ni yeye Mungu Mwenyewe ndiye aliyembele na popote awapo Mama yetu. Kwa hakika Rais Samia ameiteka mioyo ya watu.

Kwa kilichotokea Arusha, kwa mapokezi haya, kwa mafuriko ya watu ,kwa shangwe la wananchi,kwa furaha walioonyesha wana Arusha kwa Mama yetu Mpendwa ni wazi kuwa Mama ni Mtu wa Watu ,kiongozi wa watu mwenye kuaminika ,kupendwa na kukubalika.

Unajua kwanini imekuwa hivyo mpaka Kwa wana Arusha Kumpokea Rais wetu Mpendwa kwa kishindo? Jibu ni kuwa Mama Amegusa Maisha ya wana Arusha ,Hakuna aliyeachwa nyuma ,hakuna ambaye hajafikiwa na mkono wa Mama,hakuna ambaye hajaona matunda ya jasho lake,hakuna aliyeulizwa na Mama kimaamuzi au kisera au kisheria.

Kila Mwaka Arusha ameshuhudia namna secta ya utalii ilivyofanya vizuri awamu hii na kuzalisha ajira na fursa mbalimbali kwa vijana na makundi mbalimbali kuanzia Mama ntilie , bodaboda, Bajaji,waongoza watalii,wamiliki wa mahoteli na magari ya kusafirisha watalii ,machinga na wafanyabishara mbalimbali na wa biashara tofautitofauti wameona namna hali ilivyokuwa nzuri na kuongeza kipato chao awamu hii ya Mama yetu msikivu na mwenye upendo kwa watu wote.

Wana Arusha wafanyabiashara wameona biashara zao zikistawi ,kukua na kushamiri wakati huu wa Mama kuliko wakati mwingine wowote ule katika historia ya Taifa letu. Wafugaji nao pia wameona namna ambavyo secta yao ikikua na kuwaletea maendeleo. Ndio sababu ya leo hii watu kufurika na kumiminika kumlaki ,kumpokea na kumsikiliza Rais wetu Mpendwa kwa Bashasha,furaha na shangwe kubwa lililolindima na kuitetemesha kanda ya kaskazini nzima.View attachment 3482379

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Unatumia VPN?
 
Vichekesho Mungu tangu lini kafanya utekaji, kuweka wapinzani ndani na ku block
Huyu Mama ameingiwa na majini mabaya tumuombee arudi kama 2021-2022 tusiko omba hata miaka 2 hamalizi hayo hayo majini yatamuondoa
 
Masikini nimeona wafanyakazi wa Ato z wakilalamika kusombwa kwa nguvu kwenda kujaza uwanja, yaani kwa lazima upende usipende, wao tu ni zaidi ya watu elfu tano, kama unabisha kawaulizr, nimesikitika sana, nimeona wakishushwa kwenye mabasi yao yapatayo 20 hivi, wanamwagwa kisha mabasi yanarudi kusomba wengine.
Acha uongo wako na wivu hapa. Unaweza vipi somba maelfu kwa maelfu wanaojaa kwenye mikutano ya Rais wetu.
 
Vichekesho Mungu tangu lini kafanya utekaji, kuweka wapinzani ndani na ku block
Huyu Mama ameingiwa na majini mabaya tumuombee arudi kama 2021-2022 tusiko omba hata miaka 2 hamalizi hayo hayo majini yatamuondoa
Mbona wewe hujatekwa? Huna adabu wewe
 
Back
Top Bottom