Picha: Kwa uzembe kabisa Serikali isivyojali mitambo yake!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
18,653
Reaction score
31,010


Huu mtambo upo Bunju kando kando ya barabara ya Bagamoyo.
Umeharibika na umekuwa hapo karibu mwezi mmoja sasa.
Kabla ya hapo ulikuwa pale Mbezi Goig na pale vile vile ulikaa barabarani mwezi mmoja..
Huu ndo umakini wa idara za serikali-naamini huu ni mtambo wa Halmashauri fulani hapa Dar es salaam.
Magufuli baba kuna mtu anaomba kutumbuliwa, rudi DSM!

NB
Mtambo huu ukiwa mpya bei yake Tshs 400million.
UPDATE
Mtambo bado upo, mwezi na nusu sasa hapo.

 
Uzembe huu upo Tanzania nzima. Tatizo ni Magufuli mwenyewe kuyaweka yote ya mitambo kimababe chini ya TAMESA isiyokuwa na uwezo. JPM aondoke zake Oktoba 28, 2020 Hatufai.
 
Uzembe huu upo Tanzania nzima. Tatizo ni Magufuli mwenyewe kuyaweka yote ya mitambo kimababe chini ya TAMESA isiyokuwa na uwezo. JPM aondoke zake Oktoba 28, 2020 Hatufai.
Mkuu huu mtambo si wa TEMESA, ni wa Halmashauri hapa jijini.
 
Sisi ni wepesi kununua kwakuwa tunapata 10% baada ya hapo ni ku damp na kutazama fursa zingine za kupiga
Naweza amini hili.Mtambo huo unaonekana ni mpya lakini umechakaa kwa kukosa uangalizi.
Hakuna mtu binafsi anaweza fanya uzembe huo.
 

Mtoa mada nimejaribu ku zoom hiyo plate no.
Inasoma.

......57..8
 
Mkuu huu mtambo si wa TEMESA, ni wa Halmashauri hapa jijini.

Mkuu, utaratibu wa Magufuli nchi nzima ni kuwa mitambo yote ya Serikali ikiwemo Serikali za mitaa kama Halmashauri inatengenezwa na TAMESA kwa kugharamiwa na Halmashauri husika. Hapo ndipo tatizo linapoanzia. Kuna urasimu mkubwa sana TAMESA na ukosefu wa utaalamu husika. Matokeo yake mitambo mingi hutelekezwa mahali inapoharibikia iwe barabarani au garage.
 
Kweli hali hii inasikitisha.
Mtambo huu ukiwa mpya bei yake si chini ya $175,000 (zaidi ya 400million) pale Agent wao Hyundai Vingunguti.
Halafu mtambo unachakaa barabarani.
Inasikitisha.
 
Serikali ya kipigaji
 
Huo mtambo ni wa Halmashauri.
Huu mtambo una kama miaka mitano na iliuzwa n Hyunda EA, Branch yao iko pale Vingunguti.
Nikipita tena hapo bado upo nitapiga picha details za plate no.
For sure hakuna mfanyabiashara mzembe ataacha mtambo kama huo barabarani.
 


Okey, kama una uhakika kwahilo sawa huo ni uzembe wa halmashauri husika!

*lapili kuhusu kuwa hakuna mfanyabiashara mzembe anayeweza kuuacha mtambo wake barabarani, sio kweli wapo mkuu,,

Mimi ni Operator wa plant, (heavy duty machines) pamoja na hii hydraulic excavator, pia motor grader, loader, compact roller, na crane! Nimefanyakazi kwenye kampuni nyingi , wazembe wapo kaka, juzi pale mbezi salasala, karibu na mizani (jkt) pale mbuyuni, kuna kampuni binafsi iliacha mtambo wake wa motor grader karibu week!

Wazembe wapo kila sehemu mkuu,,, acha tu!
 
Kuna mungine uko huku njia panda ya tegeta A ukitokea Goba njia nne kwenda madale. Upo hapo tangu june
 
Kuna mungine uko huku njia panda ya tegeta A ukitokea Goba njia nne kwenda madale. Upo hapo tangu june
Hizo ni kodi zetu mkuu na kuna mzembe anatakiwa kutumbuliwa.Piga picha na rusha mtandaoni.
 
Nakubaliana mkuu, mitambo hii ni gharama kubwa sana.
Kuitelekeza ni uzembe mkubwa.
 
Haya ndio anayoyasema Lissu jambo dogo kama hilo nalo linasubiri Rais wa Nchi atoe tamko???
 
Nakubaliana mkuu, mitambo hii ni gharama kubwa sana.
Kuitelekeza ni uzembe mkubwa.
Hakuna cha gharama kubwa,kuna zaidi ya VXR 30 zilizo kwenye msafara wa Samia,Majaliwa,Magufuli,Pinda,Bushiru na Kikwete moja linauzwa sio chini ya 400M bado mafuta yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…