Picha: Kwa uzembe kabisa Serikali isivyojali mitambo yake!

Nenda ofisi za serikali au nenda CCM mkoa pale Lumumba ndo utaona magari mazuri yanavyoozea hapo. Mengi yao yalifikishwa pale kwa matatizo madogo tu kama kuharibika AC nk. Hawawezi hata kuuza angalau kurudisha nusu hasara. Wanasubiri yanachakaa mpaka yanaoza. Huu ni zaidi ya UPUMBAVU
 
Kodi zetu masikini.
Wawajibike!
 
Kodi zet zitumiwe vizuri wajameni.
Tukiona hivi tunaumia.
 
Kuna mungine uko huku njia panda ya tegeta A ukitokea Goba njia nne kwenda madale. Upo hapo tangu june
....Ndipo MTU unajikuta ukikubali hoja kuwa Tanzania hatuna vyombo vya Habari!

Hebu fikiri tu gazeti kama Mwananchi, Nipashe ama lingine lolote Kubwa liupige picha Mtambo huo na kuiweka Front page ikieleza ulivyotelekezwa!
Kuwa watu watajiharishia Sikh nzima na kutamani kuzinunua nakala zote za gazeti husika!
Na jioni take tu mtambo utakuwa umeondolewa na kurejeshwa mahali unapopaswa kuwa!

Bado hatujajua kutumia nguvu ya vyombo vya habari!!![emoji34]
 
Kuna tatizo kubwa sana kwenye maintenance ya vifaa na nitambo ya umma. Sometimes inauniza sana yaani unakuata mtambo umetelekezwa unaliwa na kutu tu kwa tatizo dogo sana
 
Kwenye suala la matengenezo kwenye mali za serikali kwakweli inatia huruma ukijaribu kwenda kwenye ofisi nyingi za serikali utakuta magali yako vizur tu mengi ukijaribu kuuliza utaambiwa klachi imearibika wakat wangeweza hata kuyapiga mnada waweze kuokoa japo kidogo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kaitoe haraka kabla Mtumbuaji-in-Chief hajarudi Dsm.
Na leo kaahidi jamaa kuipiga picha plate no.
Mtumbuaji hua anahangaika kutumbua madudu ya sekta nyingine tu,sekta ujenzi ndio kipenzi chake hata wafanye nini wako safe.
 
Million 400 tu na mpango wa kuzinunua hizo kama 100
 
Kuna tatizo kubwa sana kwenye maintenance ya vifaa na nitambo ya umma. Sometimes inauniza sana yaani unakuata mtambo umetelekezwa unaliwa na kutu tu kwa tatizo dogo sana
Maintanance culture haipo kabisa.
Watu wanapenda kujisifu kwa kununuakitu kipya tu.
 
Haya ndio anayoyasema Lissu jambo dogo kama hilo nalo linasubiri Rais wa Nchi atoe tamko???
Safi sana. Mwishowe tutasubiri Raisi wetu aje asimamie usafi wa ofisi zetu. Tuwajibike jamani, mtaani kugumu sana hasa if you're not pensionable
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…