GE2025 PICHA: Maelfu kwa maelfu ya Wananchi wakiongozwa na mstaafu Kikwete wamempokea kwa kishindo Rais Samia Chalinze

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan amepokelewa kishujaa kwa mapokezi mazito na ya kihistoria Chalinze Mkoani Pwani.

Ambapo katika Mapokezi hayo Maelfu kwa Maelfu ya Wananchi Wakiongozwa Na Rais wetu Mstaafu Daktari Jakaya Mrisho Kikwete Walijitokeza kwa wingi kama mchanga wa Baharini kumlaki Mama yetu Mpendwa kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Lakini pia katibu Mkuu wetu wa CCM Mheshimiwa Balozi Dkt Asha Rose Migiro Naibu katibu Mkuu Wa Umoja wa Mataifa Mstaafu naye alikuwepo katika Mapokezi hayo.

Rais wetu na Mama Yetu Mpendwa anaendelea kuonyesha Namna anavyopendwa na kukubalika machoni na mioyoni Mwa Watanzania. Anaendelea kuonyesha ni kiongozi wa watu mwenye baraka za watanzania. Anaendelea kuonyesha anaongoza Taifa na watu ambao wanamkubali ,kumpenda na Kumuamini sana. Ndio maana anasikilizwa na kukubalika kwa watu na kupata mapokezi mazito kuwahi kutokea katika historia ya Taifa letu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Your browser is not able to display this video.

APEDOM[UNYANI] , ni ajabu katika nchi ambayo usafiri katiks jiji kubwa na kitovu cha uchumi watu wanapanda usafiri wa umma kwa kudandia kama nyani halafu kuna machawa /kunguni wanakuja kumsifia mtawala huyohuyo ambaye tena ili ajaze watu kwa kuwabeba kwenye malori kama mifugo ili wafike kuona matamasha yake ya wasanii anayoyaita kampeni.

Unyani wa hali ya juu ni kumsifia mtawala ambaye ameondoa haki yako ya kutoa maoni kikatiba kwa kufungia sehemu za kutoa maoni kama X, Clubhouse na sasa jukwaa pekee la kitanzania JamiiForums.

Ni unyani wa hali ya juu kuweka kutumia funguo bandia kupita mlango wa nyuma[VPN] kuja kumsifia mtawala huyo ambaye licha ya kukuzuia kutoa maoni bado anasema ukasajili VPN yako ambayo ni kinyume na taratibu za ulinzi wa taarifa binafsi , nilizoea kuwaona nyani porini ila sasa tunaye nyani jukwaani.

Na nyani huyu wa jukwaani hapa ni mleta mada.
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Utafikiri wanyama. Na hapo hapo nje kuna bango linasema Mama Kaboresha Usafiri.

Na siku moja basi liwake moto. Watateketea watu wengi sana. Yeah!
 
Hujitambui
 

Ana neno lolote kuwahusu ndugu zetu hawa?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…