GE2025 PICHA: Maelfu kwa maelfu ya Wananchi wakiongozwa na mstaafu Kikwete wamempokea kwa kishindo Rais Samia Chalinze

GE2025 PICHA: Maelfu kwa maelfu ya Wananchi wakiongozwa na mstaafu Kikwete wamempokea kwa kishindo Rais Samia Chalinze

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Utafikiri wanyama. Na hapo hapo nje kuna bango linasema Mama Kaboresha Usafiri.

Na siku moja basi liwake moto. Watateketea watu wengi sana. Yeah!
Yaani wati wanaolipa kodi na bado wanadandia dirishani kama manyani halafu mabango na magari wanayotembelea wakusanya kodi yameandikwa "kazi na utu" hivi kwa kudandia huko utu unaweza kuwepo kwa namna gani mtoto wa miaka 12 au mzee wa miaka 60 anaweza kweli heka heka hizo?
 
Yaani wati wanaolipa kodi na bado wanadandia dirishani kama manyani halafu mabango na magari wanayotembelea wakusanya kodi yameandikwa "kazi na utu" hivi kwa kudandia huko utu unaweza kuwepo kwa namna gani mtoto wa miaka 12 au mzee wa miaka 60 anaweza kweli heka heka hizo?
Nunua gari lako na Familia yako
 
Nunua gari lako na Familia yako
Gari katika ulimwengu wa kwanza ni hitaji la msingi na sio anasa hivyo lilishakuwepo zamani

Swali langu la msingi ni huyu mama yenu anaweza kupull crowd bila kusomba watu kwenye malori.

Kwa mfano yani wewe unaweza kumsikiliza Samia , saa nzima akiwa anazungumza?

Kwanza hajui public speaking , hana mvuto wa uzungumzaji na pia kupangilia mazungumzo yake na anakuwa na afadhali akiandikiwa hotuba kuliko akiwa anatolea kichwani .

Akitolea kichwani ndio anakuja na misemo kama nywinywii nywanywanywa, jitu ,kudemka na vitu vingine visivyo na tija.

Hebu msikilize hapo Mkapa walau kwa dakika chache japo najua lugha hiyo kwako ni changamoto , pia jaribu kupitia comments na ufananishe na hotuba za Samia utaona jinsi ofisi ya rais ilivyoshuka viwango yaani hata Baba Levo au Kingwendu wanaweza kuwa marais ili mradi awe anajua kuiba kura tu.


View: https://youtu.be/XN19XsgU9Es?si=mKYT20MmRKIHm5xZ

Kuna siku hadi anaanza kuongelea habari za vifua vya wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake kuwa vinafanana na wanaume hivyo wanaweza kukosa wachumba unajiuliza hivi ni vitu rais anavizungumzia kabisa mbele ya umma kwani hakuna mambo mengine ya msingi?
IMG-20250831-WA0001.jpg

 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan amepokelewa kishujaa kwa mapokezi mazito na ya kihistoria Chalinze Mkoani Pwani.

Ambapo katika Mapokezi hayo Maelfu kwa Maelfu ya Wananchi Wakiongozwa Na Rais wetu Mstaafu Daktari Jakaya Mrisho Kikwete Walijitokeza kwa wingi kama mchanga wa Baharini kumlaki Mama yetu Mpendwa kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Lakini pia katibu Mkuu wetu wa CCM Mheshimiwa Balozi Dkt Asha Rose Migiro Naibu katibu Mkuu Wa Umoja wa Mataifa Mstaafu naye alikuwepo katika Mapokezi hayo.

Rais wetu na Mama Yetu Mpendwa anaendelea kuonyesha Namna anavyopendwa na kukubalika machoni na mioyoni Mwa Watanzania. Anaendelea kuonyesha ni kiongozi wa watu mwenye baraka za watanzania. Anaendelea kuonyesha anaongoza Taifa na watu ambao wanamkubali ,kumpenda na Kumuamini sana. Ndio maana anasikilizwa na kukubalika kwa watu na kupata mapokezi mazito kuwahi kutokea katika historia ya Taifa letu.View attachment 3480442View attachment 3480443

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

View: https://youtu.be/vTA2KJ_cyA4?si=hbe0wanUFYbkdW1I
 

Attachments

  • SHEKH ATOA SIRI ZOTE SABABU YA RAIS SAMIA KUOGOPA KUNG'ATUKA.#millardayo #globalonline #sns..mp4
    6.4 MB
Back
Top Bottom