Picha Mahakama Kuu Zanzibar - jengo latia aibu

Picha Mahakama Kuu Zanzibar - jengo latia aibu

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
ase3.JPG


ase.JPG


Wakuu wa nchi wako busy na misafara huku kisima cha kuchota pesa za kusafiria hakikauki wakati baadhi ya majengo ya mmoja ya mhimili wake yakiwa hoi na yanatia kichefuchefu. Gharama ya kukarabati isipofanyika hima itatugharimu walipa kodi kujenga jengo jingine kwa mabilioni. Hali hii wahusika waniona?
 
Majengo mengi ya SMZ hali hiyo hiyo with exception central bank, migration na wizara ya elimu.
 
Hayo ni majengo ya kihistoria hayapaswi kubadirishwa yanaachwa mpaka yaanguke kabisa. Hivyo ndivyo nionavyo mimi kuwa labda ndio sababu inawafanya wayapotezee. Ama kwa upande mwingine naweza sema kuwa hayarekebishwi kwa kuwa viongozi hawashitakiwi,wangekuwa wanashitakiwa viongozi wakuu basi pangesafishwa .
 
Mi mwenyewe nimeshangaa majengo ya ajabu kabisa.Hawa ndg zetu na hilo watalaumu muungano!
 
Jengo hilo waulizeni Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe!
 
Mambo ya mahakana isipokuwa mahakama ya Rufaa tu ndo mambo ya muungani
 
aiseeeeeeeee babaangu mpaka lianguke liuwe watu ndio watarekebisha

nawasi nawasilisha kweli
 
Mambo ya mahakana isipokuwa mahakama ya Rufaa tu , sio mambo ya muungano
 
wazenji wenyewe walivyo na dharau wacha wakae hivo hivo..hakuna kuwasaidia
 
Duh gofu hilo kumbe wana sababu za msingi muungano hauwanufaishi wao
 
Muonekano wa ndani ni tofauti na nje au macho yangu yananidanganya?
 
Duh gofu hilo kumbe wana sababu za msingi muungano hauwanufaishi wao


ase3.JPG


Mwonekano wa jengo kuchuja, kuvuja na mengineyo kwa kiwango hiki hata wanaofanya kazi hapo sijapata picha wanajisikaje. Aibu tupu hata kumwonyesha mtu kwamba wafanya kazi hapo ni kina kubwa la Mahakama ambalo ukitazama jengo unaishiwa nguvu.
 
Stone town yote haitakiwi kuvunja jengo bila kibali. hilo jengo ni rangi 2 bado liko fresh kabisa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Watapata habari kuwa "wamesemwa JF". Baada ya mwezi utaona Gofu hilo linapakwa rangi.

UNESCO wanapenda uhifadhi wa majengo ya kihistoria, mdau mmoja awatonye UNESCO.
 
Watapata habari kuwa "wamesemwa JF". Baada ya mwezi utaona Gofu hilo linapakwa rangi.

UNESCO wanapenda uhifadhi wa majengo ya kihistoria, mdau mmoja awatonye UNESCO.

Kesi ya uamsho imesaidia kuibua watu kujua mahakama kuu ya Zanzibar iko kwenye jengo ambalo ni govu.
 
Back
Top Bottom