Picha: Makazi ya kwanza tuwapo Mars

Picha: Makazi ya kwanza tuwapo Mars

isajorsergio

Platinum Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
4,143
Reaction score
6,560
Kuanzia 2022 na 2024 baada ya kufika kwetu katika sayari ya Mars, tutaanza kwa kuishi katika makazi ya namna hii huku tukiitransform Mars kuwa nzuri zaidi.

3.png


Picha ikionesha majengo yaliyojengwa kwa teknolojia ya 3D Printing.

2022 na 2024 tukifika kuanza shughuli za ujenzi na utafiti akinifu katika sayari ya Mars basi tutahitaji Makazi wezeshi tuwapo huko.

Kutokana na kuwapo baadhi ya changamoto kama miale na mionzi mikali, upepo, vumbi, joto na baridi kali yatokanayo na kutokuwepo uoto wa asili. SpaceX na ushirika wa makampuni na mashirika yapatayo 21 imefikia makubaliano ya kuunda makazi wezeshi kwa kuanzia tuwapo Mars.

Tayari makubaliano ni utuamiaji wa mfumo 3D Printing Technology tuwapo Mars kuweza kuendana na muda na kukamilisha mipango mkakati, teknolojia ya 3D Printing itatolewa kiukamilifu na ndugu zangu AI Space Factory huku usanifu wa majengo ukitolewa na Marshal pamoja na Terra Space.

Hivyo ujenzi wa 3D Printing utafanyika na utengenezwaji wa bowl's zilizo upside down zitakamilika na hapo tutatia maputo maalum ndani ya bowl's hizo na vifaa tayari kwa nyumba, ofisi na labs zetu tukiwa huko.

Hivyo mionzi, upepo, joto na baridi tutakuwa tumeweza kupambana navyo kwa muda huo tukiandaa mazingira kabla ya Terra kuja na majengo lengwa ya taifa hili la Mars.

Wakati huo usimikaji wa Panels kwa ajiri ya nishati wezeshi utakuwa tayari hivyo kufanya mji wetu kuwaka na kutoa huduma kwa watu tutaokuwapo huko.

Kama picha inavyosadifu kuna hati hati ya mimi kuwa katika hilo jengo la kijani huku nikizungukwa na majengo kama mnavyoona yakiwa na mwanga.

Picha kwa hisani ya isajorsergio Space na isajorsergio Studios.

- Sergi 🐰
 
Oxygen asilimia ngapi huko ukilinganisha na huku?

Mpango wa kurekebisha anga hewa huko umefikia wapi?
 
Mtuwekee tu pahala pa kutekeleza ibada bila hivyo patachimbika.
 
Oxygen asilimia ngapi huko ukilinganisha na huku?

Mpango wa kurekebisha anga hewa huko umefikia wapi?
 
Last days, Mzungu anaamini ataikimbia adhabu kwa kwnda sayari nyingne ila anasahau there will only be lake of fire na heaven and nothing else.

Sent using Jamii Forums mobile app
ingekuwa kwenda huko basi mwili haufi, duniani wangebaki wachache sana hata wanaojiita watumishi mitume na manabii wanaoona kufa katika yesu ni uzima nao wangepakimbia hapa duniani
 
Hivi huko Mars Israel mtoa roho yupo!!?

Sent from my Nokia 6.1 Plus using Tapatalk
 
Back
Top Bottom