Picha: Mfahamu kwa undani muigizaji "ODAMA"

Picha: Mfahamu kwa undani muigizaji "ODAMA"

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Anaitwa Jennifer Kyaka, ila wengi wamezoea kumuita ODAMA, jina ambalo liliibuka kwenye movie ya Odama aliyoigiza, ambapo yeye alicheza kama mhusika mkuu. Alizaliwa mnamo mwaka 1983 jijini Mwanza katika Hospital ya Bugando.

Safari yake ya sanaa ilianza mnamo mwaka 2006, na movie yake ya kwanza kuigiza ilikuwa inaitwa SHUMILETA, Movie iliyoandaliwa na producer na director maarufu nchini, Mussa Banzi, watu wengi walianza kumfahamu kwenye movie hiyo ya kutisha aliyocheza kama Monte.

Movie ya Shumileta ilimfungulia milango, ambapo mrembo huyo asiye na makuu alianza kuonekana kwenye movies kadhaa ikiwemo, ODAMA, BEYONCE, VERONICA, BROKEN HEART na nyinginezo.

Jina lake likazidi kukua, watu wakamtambua zaidi kutokana na kipaji na uhodari wake wa kuigiza kwa hisia za hali ya juu na kuuvaa uhusika vilivyo ,movie kama ODAMA na VERONICA zinatajwa kuwa miongoni mwa movie zilizomuweka muigizaji huyo kwenye ramani nzuri kwenye sanaa , haswa kutokana na uhalisia alioubeba kwenye movies hizo.

Baadae aliamua kuandaa movies zake mwenyewe kupitia kampuni yake ya J-FILM FOR LIFE, ambapo ndani ya kampuni hiyo alitengeneza movies zisizopungua 30, movies kama LIFE 4 LIFE, LOREEN, CHOCOLATE, RUDE, PAIN KILLER, WHITCH DOCTOR, INSIDE, JICHO LANGU na JADA ambayo mpaka sasa ivi inafanya vizuri sokoni kwa mauzo.

Muigizaji huyo ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, anatajwa kuwa ni miongoni mwa producers wenye mpunga mrefu apa nchini, japokuwa mwenyewe hataki kujionyesha kuwa anazo. Pia anatajwa kujenga nyumba na kumiliki magari kadhaa pamoja na kampuni na kumiliki biashara, ni moja ya mafanikio anayojivunia muigizaji huyo mwenye uzuri wa asili na mvuto wa aina yake.

Written and prepared by warumi

Copy with acknowledgement!!
 
Muigizaji jennifer kyaka (ODAMA )
 
Attachments

  • 1427021286873.jpg
    1427021286873.jpg
    63.1 KB · Views: 2,017
Nasikia hana kizazi Odama.
Watu walimvuta baada ya kumfumania na mume wa mtu.
Binamu thibitisha
 
Nasikia hana kizazi Odama.
Watu walimvuta baada ya kumfumania na mume wa mtu.
Binamu thibitisha

Eeehh binamu mbona sijaupata huo umbea jamani? Ila mbona ana mtoto lakini? Hilo sakata limemkumba lini??
 
Eeehh binamu mbona sijaupata huo umbea jamani? Ila mbona ana mtoto lakini? Hilo sakata limemkumba lini??

Huyo huyo mwanaume aliyezaa nae, nasikia mume wa mtu.
Watu wakamuundia zengwe....sijui ikawaje mpaka kizazi kikachoropoka.
Ila binamu mji huu, kama fulani hampendi mtu, atazushiwa maneno mpaka atalijua jiji
 
Eeehh binamu mbona sijaupata huo umbea jamani? Ila mbona ana mtoto lakini? Hilo sakata limemkumba lini??

mkuu,hvi huwa una ma agents wa kukupa umbea au hzi habari za watu huwa unazitoa wapi?
 
Huyo huyo mwanaume aliyezaa nae, nasikia mume wa mtu.
Watu wakamuundia zengwe....sijui ikawaje mpaka kizazi kikachoropoka.
Ila binamu mji huu, kama fulani hampendi mtu, atazushiwa maneno mpaka atalijua jiji

Huo umbea wa kuzaa na mume wa mtu unajulikana, ila hyo ya kizazi mmh bado mpya kwangu, uliyasikia wapi binamu? Tusije kusutwa mwenzangu na jumapili yote hii na mvua hii, ni balaaaaa ahahahahahaj
 
mkuu,hvi huwa una ma agents wa kukupa umbea au hzi habari za watu huwa unazitoa wapi?

HUmu kuna watu wanajua mambo mengi zaidi kuliko mimi, so kwa namna moja au nyingine tuna habarishana na habari nyingine uwa natafuta mwenyewe uko kwenye vijiwe vya umbea cc Dinazarde
 
Last edited by a moderator:
Ucngeweka picha ningebaki nawaza uzr wake ulipoweka picha kumbe wa kawaidavkabsa
 
Haya sawa basi, nimemfahamu tayari...! Weka pia ya MARIAM MBEWA ambaye naye yupo vizuri nasikia tu
 
Binti yuko vizuri, ila inabidi awe anatembelea gym ili aunguze excess body fat. Nilimuona this week nje ya office za Steps Mtaa wa Masasi Kariakoo. Zaidi ya hapo yuko fresh, hususan miguu yake.
 
Back
Top Bottom