POTOSHI Picha: Mkuu wa Kituo cha Polisi Kabwe Wilayani Nkasi ajeruhiwa na Wananchi

POTOSHI Picha: Mkuu wa Kituo cha Polisi Kabwe Wilayani Nkasi ajeruhiwa na Wananchi

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimekutana na hii taarifa kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa mkuu wa kituo cha polisi huko Nkasi mkoani Rukwa amejeruhiwa na wananchi ambapo mpaka sasa wananchi takriban 76 wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tukio hilo pamoja na kuharibu mali wakati wa tukio hilo.

WhatsApp Image 2024-12-11 at 10.58.00_46ba45ab.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na Picha inayodaiwa kuwa ya Mkuu wa kituo cha Polisi cha Kabwe kilichopo Wilayani Nkasi ambapo Taarifa hiyo inasambaa mitandaoni (Tazama hapa hapa)

whatsapp-image-2024-12-11-at-10-58-00_46ba45ab-jpg.3174267

Je, Uhalisia wa Picha hiyo ni Upi?

JamiiCheck imefatilia Picha hiyo na kubaini kuwa picha inayodaiwa kuwa ya Mkuu wa Kituo cha Kabwe cha Wilaya ya Nkasi si ya Tanzania.

Mnamo Oktoba 18, 2021 Times Live ya Afrika Kusini walitoa Taarifa ya Mwanaume Mmoja ambaye ndiye anayeoonekana pia kwenye picha inayosambazwa kuwa kama Mkuu wa kituo cha Nkasi, Times Live walidai Mwanaume huyo alijitambulisha kwa jina Moja tu la Shiba, ambaye alikuwa akiwatuhumu Jeshi la Polisi la Afrika Kusini kwa kumshambulia ambapo walieeleza kuwa Polisi 11 walikuwa wanashikiliwa kwa tukio ambalo lilidai kushambuliwa kwa watu 3 akiwamo mwanaume huyo. (Soma hapa)

Aidha, Dispatch Live waliripoti Taarifa kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 2, 2021 Majira ya Saa 5 usiku, wakati watu hao watatu akiwemo mwanaume huyo walipokwenda kwenye kituo cha Tshwane kilichopo Madiba Street, wakitaka kuchukua gari lao. Aidha wanadai Taarifa hiyo ilianza kusambaa mtandaoni kwa kasi Oktoba 6 2021.
1733917296734-png.3174438
Aidha, Taarifa ya kushambuliwa kwa Mkuu wa Kituo cha Kabwe cha Wilaya ya Nkasi iliripotiwa kutokea Septemba 11, 2023 ambapo kwa mujibu wa Kamishina Msaidizi wa Polisi, Shedrack Masija, watu 76 walishikiliwa kufuatia tukio hilo, ambapo kwenye Taarifa hiyo Jina la Mkuu wa kituo wala Picha yake havikutolea kama ilivyoripotiwa na Mwananchi Septemba 15, 2023

Hivyo, wanaoihisisha picha ya Shiba na Shambilio la Mkuu wa kituo cha Kabwe wanafanya upotoshaji kwani Shiba alishambuliwa Oktoba 2, 2021 ambapo picha zake zilianza kusambaa Oktoba 6 2021 na Mkuu wa Kituo cha Kabwe alishambuliwa Septemba 11, 2023

Vilevile, picha ya gari inayoonekana mbele ya Shiba inathibitisha kuwa hapo Si tanzania, kwani gari inayoonekana hapo ina Nenbo ya Jeshi la Polisi ya Afrika Kusini.
Back
Top Bottom