mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 1,155
- 2,704
Julai 16, 2026, Msemaji wa Serikali ya Tanzania kupitia ukurasa wake wa Instagram alichapisha:
"Diaspora anayejua kupigania bendera ya Tanzania na manufaa ya Watanzania kwa vitendo namzungumzia @johnjackson_jj amemfikia mwanamziki mkubwa na maarufu nchini Marekani @djkhaled
@johnjackson_jj hakukutana na @djkhaled ili kulalamika, au kuisema vibaya Tanzania, au kuomba Wasanii wakubwa wasije Tanzania, au kuponda Watalii wasije Tanzania au kupigia chapuo propaganda za kimagharibi dhidi ya Tanzania. Amemkabidhi jezi ya Taifa Stars na kisha akamshawishi na kumkaribisha DJ Khaled kuja Tanzania kutembelea vivutio vya utalii ili Watanzania wapate pesa na nchi ipate pesa za kutoa huduma kwa wananchi.
JE WEWE DIASPORA ULIOPO MAREKANI, UINGEREZA, ULAYA YOTE, BRAZIL, MASHARIKI YA KATI, AUSTRALIA, CHINA n.k ukikutana na fursa kama hizi huwa unapiga picha za kutambia mtaani? za kuombea connections zako binafsi? za kujifanya wewe sio Mtanzania? za kutukuza ukoloni? au za kupenyeza ajenda za kuinufaisha nchi yako?
Huyu ni Diaspora wa maana kabisa. JOHN JACKSON UMEPOA!!!!! UMEPOA!!! UMEPOA!!!!, sema halaa!!!"
Kufuatia chapisho hilo la Gerson Msigwa, jana Julai 23, 2026 kupitia ukurasa wa Instagram wa michaelyormark ilichapishwa taarifa ikikanusha madai yaliyotolewa na Msigwa na kwamba Dj Khaled hana makubaliano yoyote na 'Visit Tanzania' na kwamba jitihada zinafanyika ili maudhui ya hayo yaondolewe.
Taarifa hiyo ilisistiza kwamba washiriki halali ni 'Explore Rwanda'
"Roc Nation Sports International is aware of unauthorised content circulating online falsely portraying an endorsement deal between DJ Khaled and Visit Tanzania.
This content is unapproved and constitutes IP infringement - no official endorsement exists.
Active legal and administrative measures are currently being taken to enforce the prompt removal of this content and end all false representation.
OUR REAL PARTNER IS EXPLORE UGANDA."