Wewe unaamini picha ya kuchora??? Kumbuka mchoro huchorwa kwa mujibu wa maelezo ya walioshuhudia tukio. Sasa yawezekana mtoa maelezo akawa hana elimu sana ya kujua namna ya kutoa maelezo. Mfano, mtu akiulizwa mtu huyo ni mweusi au mweupe? Akajibu ni mweupe kumbe yeye alimaanisha weupe tunaoujua sisi katika wajihi wa mwanadamu yaani maji ya kunde. ama akaulizwa mtuhumiwa ni mrefu ama mfupi yeye akasema mfupi kumbe hajui mtuhumiwa ni mrefu ila kwa kuwa alikuwa kakaa kwenye pikipiki ndo maana ameona kuwa ni mfupi etc etc. Mimi naamini sana ushahidi wa kumkamata mtuhumiwa katika eneo la tukio kabla hajakimbia. Hapo huwa sina ubishi ingawa sheria ya ushahidi napo pia huwa kuna ka-ugumu kake ka ku-provu.
Maelezo wanayotoa wanaoulizwa na wachoraji hutegemea sana na namna wanavyoulizwa maswali na wachoraji. Wanaweza wakawa na lengo la kufanya uchunguzi haraka hivyo kutaka walioushudia tukio hilo kutoa ushahidi wa haraka ili kutoa ripoti. Yawezekana mtoa maelezo akatoa maelezo yanayomuhusisha mtu mwingine kabisa, yaani picha itakayopatikana kutokana na malezo ikawa ni ya mtu mwingine asiyehusika. Kwa mfano, maelezo waliyoyapata FBI na mchoro uliotengenezwa vingefanana na DPP ingekuwaje hapo? Kumbuka wabongo huwa si wazuri sana katika kutoa maelezo kwa kimombo, sasa sijui FBI walitumia lugha gani?