SI KWELI picha na video hizi ni za matukio yanayoendelea nchini kenya?

SI KWELI picha na video hizi ni za matukio yanayoendelea nchini kenya?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kumekuwa na video zinazosambazwa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa kumefanyika maandamano nchini Kenya kupinga hatua ya Serikali ya kuwaondoa wageni wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo nchini humo.

kenya.jpg

 
Tunachokijua
Kumekuwa na video zinazosambazwa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa kumefanyika maandamano nchini Kenya kupinga hatua ya Serikali ya kuwaondoa wageni wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo nchini humo.

Video hizo zinaonyesha baadhi ya waandamanaji wakipinga hatua zinazodaiwa kuchukuliwa na Rais wa Kenya, William Ruto.

Baadhi ya video hizo zimechapishwa kupitia hapa, hapa , hapa

Hata hivyo, kupitia ufuatiliaji wa chanzo cha video hizo kwa kutumia Google Reverse Image Search, imebainika kuwa baadhi yake zinaonyesha matukio ya zamani na si maandamano ya sasa ya kupinga hatua ya Serikali ya Kenya kuwaondoa wageni wanaofanya biashara ndogo ndogo.

Baadhi ya video hizo zimeonekana kuwa za maandamano yaliyofanyika nchini Kenya mwaka 2024, wakati wananchi walipopinga Mswada wa Fedha (Finance Bill) uliokuwa ukipendekezwa na Serikali.

Hata hivyo, katika hali inayoendelea nchini Kenya, Serikali imewapa wafanyabiashara wa kigeni muda wa siku 90 kuhalalisha shughuli zao za kibiashara pamoja na hadhi yao ya uhamiaji.

Katika hatua zingine baadhi ya video zimeonekana kuwa siyo matukio ya hivi karibuni bali ni matukio ya nyuma ambayo kwa sasa yameanza kuhusishwa na kile ambacho kinatokea nchini kenya
sambamba na hilo kumekuwepo na matumizi ya picha ambazo zinatumika kuonyesha matukio ya sasa huku uhalisia ukiwa ni matukio ya zamani


Hatua hiyo imekuja baada ya Rais William Ruto kutangaza msako dhidi ya wageni wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo nchini humo, jambo lililosababisha hofu miongoni mwa raia wa Burundi na mataifa mengine ya Afrika Mashariki wanaoishi Kenya.

Kwa mujibu wa masharti hayo, raia wa kigeni wanaoendesha biashara nchini Kenya wanatakiwa kuhakikisha kuwa wana nyaraka halali za uhamiaji, vibali vya kufanya kazi, usajili wa biashara pamoja na leseni zinazohitajika ili kuendelea na shughuli zao. Serikali ya Kenya imesema itaanza kutekeleza kwa ukamilifu masharti hayo baada ya muda wa siku 90 kumalizika.

Tangazo hilo limekuja wakati ambapo mamia ya raia wa Burundi walipofurika katika Ubalozi wa Burundi mjini Nairobi wakihitaji nyaraka za kusafiria, huku baadhi yao wakijiandaa kuondoka nchini Kenya. Baadhi yao pia wameripoti kukumbana na vitendo vya unyanyasaji katika siku na wiki za hivi karibuni.

Serikali ya Kenya imeomba radhi kwa raia wa Burundi waliokumbana na changamoto hizo, huku ikisisitiza kuwa hakuna marufuku ya jumla dhidi ya wageni nchini humo. Serikali imeeleza kuwa hatua zinazochukuliwa zinalenga kuhakikisha kuwa wageni wanaofanya biashara nchini Kenya wanazingatia sheria na taratibu za uhamiaji, ajira na uendeshaji wa biashara.
Back
Top Bottom