Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu lazima anarusha za kichina china. Huuu haaaa tiiff. inavyoelekea ni mlemavu, alikuwa anarusha maneno ya kashfa kwa mgombea fulani au wakati mwenge unapita. wazee wa Ukonga walipomkabili akawaonyesha kuwa naye yumo.
![]()
CCM wameshindwa kutoa nafasi kwa wananchi kuwahoji ahadi zilizotolewa 2005 na nguvu za ziada inabidi zitumike kuwazima kama ktk picha:
Juma Ramadhani (chini ya ulinzi) ambaye ni mkazi wa Nane Nane , Manispaa ya Morogoro , ambaye ni mlemavu wa viungo akizolewa msobe msobe na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia ( FFU) ambao wakisaidiana na Green Guard wa CCM . Sekeseke hilo lilianza mara baada ya Juma kudaiwa kutaka kumwona Mgombea Urais kwa Chama chama CCM,Mh Jakaya Kikwete kwa nguvu bila kufuata utaratibu , wakati huo Mh Jakaya alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni , kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini humo mwishoni mwa wiki.Picha kwa hisani ya Burudan Mwanzo - Mwisho.
Bila maelezo..nadhani utasema ni unyanyasaji wa hali ya juu wa raia tena mlemavu..lakini maelezo ya picha yatafanya watu wasitoe mawazo kwa uhuru coz watakuwa wameshajua nini chanzo cha kubebwa hivyo...
pamoja na yote,nadhani utaratibu ukifuatwa haya hayatokei na hasa unapotaka kumwona kiongozi wa nchi.
Unasemaje juu ya utumiaji wa nguvu nyingi kuliko zinazohitajika?
Askari polisi wametumwa kumlinda mgombea wa chama tawala kwa kila hali na ikiwezekana hata kutotumia akili kidogo walizonazo. Hawajui haki za binadamu hawajui elimu ya uraia.
Hivyo watu kama hawa wanaowaburuza walemavu, wanaweza kuwa na akili ya kuamini kuwa CCM imeshindwa kura? Ina maana wako tayari kutekeleza amri yoyote itakayotoka kwa bosi wao.
So sad, Tungoje Oktoba 31.
Nijuavyo mimi, Polisi kwa kawaida huwa hawatumii akili kabisaaaaaaaaaaa
Do we have Human Rights Activists here??..:confused2:
Bila maelezo..nadhani utasema ni unyanyasaji wa hali ya juu wa raia tena mlemavu..lakini maelezo ya picha yatafanya watu wasitoe mawazo kwa uhuru coz watakuwa wameshajua nini chanzo cha kubebwa hivyo...
pamoja na yote,nadhani utaratibu ukifuatwa haya hayatokei na hasa unapotaka kumwona kiongozi wa nchi.
Nijuavyo mimi, Polisi kwa kawaida huwa hawatumii akili kabisaaaaaaaaaaa
Du wanatumia nini mkuu kama hawatumii akili?
Askofu, bwana asifiwe, hao unaowaulizia kama wapo wanajadili haki za watu wenye ulemavu wakati walengwa wanachangiwa na mapolisi. Tatizo la Tanzania ni hilo tutataua matatizo mezani, field hatuendi kabisa. Na hakuna kiongozi atakayelaani hili tukio si raisi, ofisi yake , wizara inayoshughulikia wenye ulemavu, jeshi la polisi na hata wanaharakati.
Waombee ili wajue kuwa watendalo ni dhambi.
Ndio maana wana amri kuwa unaekeleza kwanza halafu unauliza baadaye, which is quite weird.
Nijuavyo mimi, Polisi kwa kawaida huwa hawatumii akili kabisaaaaaaaaaaa