Picha: Ni Ujumbe Gani Unaupata Kwa Picha Hii?

Picha: Ni Ujumbe Gani Unaupata Kwa Picha Hii?

2.JPG

CCM wameshindwa kutoa nafasi kwa wananchi kuwahoji ahadi zilizotolewa 2005 na nguvu za ziada inabidi zitumike kuwazima kama ktk picha:
Juma Ramadhani (chini ya ulinzi) ambaye ni mkazi wa Nane Nane , Manispaa ya Morogoro , ambaye ni mlemavu wa viungo akizolewa msobe msobe na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia ( FFU) ambao wakisaidiana na Green Guard wa CCM . Sekeseke hilo lilianza mara baada ya Juma kudaiwa kutaka kumwona Mgombea Urais kwa Chama chama CCM,Mh Jakaya Kikwete kwa nguvu bila kufuata utaratibu , wakati huo Mh Jakaya alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni , kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini humo mwishoni mwa wiki.Picha kwa hisani ya Burudan Mwanzo - Mwisho.
2.JPG


Picha inaonyesha kuwa Kikwete na serikali yake ni kipenzi cha wenye ulemavu
 
inaonekana kuwa serikali inamsaidia huyu mlemavu huenda ameshindwa kutokana na kukosa usafiri wa uhakika.

Tafakari chukua hatua!!!!!
 
Duhh mwajua hiyo ni kumdhalilisha mwanadamu??

Jana Skynews walitoa picha ya Askari akimburuza mama mmoja na kumweka sero ati kwakuwa mama huyo alikataa kupimwa alcohol test na huyo askari akaonekana kwenye CCTV za hapo officen kwao na huyo askari akahukumiwa kifungo cha miezi 6 kwa kumburuza tu huyo mama,
Hapa kwetu ni kazi bure na kujazana machungu na chuki baina ya raia na askari wetu ila siku sheria ikichukuwa mkondo wake hata pia raia nao watanyooka watakuwa sio wakorofi, kanini nasema haya huko marekani ukiambiwa na askari lala chini au mikono juu ni unatii amri ukizembea au kukataaa na umeisha bembelezwa ni risasi inafuatia
 
Na kuhusika kwa huyo GREEN GUARD wa CCM je. Imekaaje?
 
Tatizo la tanzania yetu hii shule ukiwa full kilaza mahali pa kujikomboa ni ajira za polisi tofauti na nchi za wenzetu field kama hiyo unapangiwa kutokana na higher qualifications ulizoarchive ukiwa shuleni na hata vyuoni.sasa sisi kwanza asilimia tisini police wameingia kwa kufoji na kununua vyeti.anayebisha abishe nimlipue.
 
Back
Top Bottom