hongera sana kwa uamuzi wako
kila mwanzo ni mgumu ila utafika tu, pitia uzi unaitwa kwa wafugaji kuku wa kisasa, pia mtafute kichwa mbovu anatoa darasa ameeleza vizuri, kutokana na picha yako nakushauri
1. funika drinkers pia jaribu kupunguza weka ratio ya 1 drinker kwa kuku 50 nadhani kwa chakula pia, jaribu kuvipanga vizuri ili uweze kupita na kuku kuvifikia
2. wawekee maranda kwani kuku wanahitaji joto vilevile yanasaidia wasiwe na direct contact na vinyesi vyao, kuku hawataki ubichi kabisa jitahidi wawe ktk hali ya ukavu muda wote
3. ili kutunza joto na pia kupunguza gharama ya maranda nk, kwa vile wadogo unatakiwa uwaweke kwenye eneo dogo na hii itawezekana kwa kuwazungushia chochote hata hayo mabox waliyokuja nayo kwenye kona ili watunze joto na wakifikie chakula na maji kwa urahisi, nimejaribu kutafuta picha zangu za vifaranga sina nakuwekea hii toka mtandaoni. Kuna kitu wanaita brooder kukuwezesha kuwakusanya eneo dogo hadi wiki ya tatu wakiota mabawa na hawahitaji joto
4. taa za chemli kama umezipenda sawa tu lakini siku hizi kuna hizi tochi mchina kwa ajili ya mwanga unaitundika juu na unaweza kuwaongezea joto kwa gai la mkaa au dumu la maji ya moto maana wanavyozidi kukua wanarukaruka hizo taa chini....
Nakutakia kila la heri na kumbuka usafi vyombo kuoshwa na sabuni kila masaa 12, chanjo na madawa kwa wakati pia chakula sahihi kwa kila stage
Asante sana mama joe! mungu akubariki na ushauri wako wote nimeuzingatia!
Hongera!!! Mungu akubariki katika biashara yako
Mbona umeweka jiko la mkaa mkuu? Hawataungua?
habari wanajamvi!
Kupitia jukwaa hili nimeamua kuanza kufuga kuku wa mayai na kwa kuanzia nimeanza na vifaranga 250 naomba nipeni ushauri jinsi nilivyoanza kuwalisha hao vifaranga kama picha inavyoonkana. Asanteni.
Updates.
Nawashukuru sana kwa wale wote walionipa ushaurii na kunitia moyo! Sasa ni mwezi wa pili na maendeleo ni mazuri sana kwani kati ya vifaranga 250 vimekufa 4! So far! Kwa kuwa nimetambua mambo mengi ambayo kwa ukweli bila kujaribu huwezi kuyajua nimeamua kuongeza idadi kamaya mwanzo ili nizidi kujikongoja!View attachment 87354
pichaView attachment 87425
jitahid vyombo vya chakula na maji viwe juu uvifunge kwa kutumia kamba.hii itasaidia kuwaepusha kuku wasile kinyesi chao kitu ambacho ni hatari sana...,.bip up kwa mradi mzuri.zingatia chanjo zote.......
Kweli hilo joto lake ni kabambwe,
sasa mkuu kwanini umetoa vile vifuniko vya juu kwenye vyombo vya chakula na maji naona inabidi ufunike ili wasikanyage kwenye maji na kwenye chakula mkuu.
pia chakula naona chombo kimoja tu au chakula kingine umemwaga chini mkuu,
yaani weka kila baada ya maji kifuate chombo cha chakula.
pia hayo maboxi ulotoa vikuku kama vipi yahamishe humo bandani.
Vinginevyo nakutakia kila la kheri na mafanikio mengi.
Kwanza honhera sana kwa kuanza ila naona umewatandazia magazeti, sijui sababu au ulikosa malanda ya mbao au magazeti ndo yanafaa vifaranga au ni sababu za kiusafi zaidi?
Naombeni kujuzwa
Habari wanajamvi!
kupitia jukwaa hili nimeamua kuanza kufuga kuku wa mayai na kwa kuanzia nimeanza na vifaranga 250 naomba nipeni ushauri jinsi nilivyoanza kuwalisha hao vifaranga kama picha inavyoonkana. Asanteni.
UPDATES.
Nawashukuru sana kwa wale wote walionipa ushaurii na kunitia moyo! sasa ni mwezi wa pili na maendeleo ni mazuri sana kwani kati ya vifaranga 250 vimekufa 4! so far! kwa kuwa nimetambua mambo mengi ambayo kwa ukweli bila kujaribu huwezi kuyajua nimeamua kuongeza idadi kamaya mwanzo ili nizidi kujikongoja!View attachment 87354
PICHAView attachment 87425
kajansi habari za leo
mradi wako wa kuku wa mayai unaendeleaje?