Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
John Paul Mwirigi, ndiye mbunge mwenye umri mdogo zaidi nchini Kenya, alichaguliwa akiwa bado Mwanafunzi wa Chuo Kikuu.
Bw. Mwirigi alitumia baiskeli na pikipiki za kusafirisha abiria, maarufu kama bodaboda, kuwafikia watu wakati wa kampeni.
Pesa nyingi alizotumia wakati wa kampeni alizipokea kutoka kwa wahisani.
Wakati wa kuapishwa alitumia magari ya uchukuzi wa umma kufika majengo ya Bunge jijini Nairobi.
Wabunge walipoalikwa Ikulu, alipewa lifti na Mbunge mwenzake.
Hata hivyo wakati wa kuondoka alitumia gari la uchukuzi wa umma maarufu kama matatu.
"Nimetimiza ahadi yangu kwa mbunge kijana wa Igembe Kusini John Paul Mwirigi katika Ikulu ndogo ya Sagana", alisema Rais Kenyatta.