Picha: Sababu na madhara ya injini kuchemsha

Picha: Sababu na madhara ya injini kuchemsha

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2018
Posts
358
Reaction score
675
SABABU ZA INJINI KUCHEMSHA na MADHARA YAKE

Na Kimomwe Motors (T) Ltd- Waagizaji Magari.

1. Maji ya kawaida haswa yenye chumvi yasiyo na Coolant. Hii inaweza tengeneza kutu ambayo hua kama tope na mwisho kuziba njia za maji katika rejeta yako.

2. Kutofanya kazi kwa feni. Inawezasababishwa na tatizo la fuse au waya za feni kuchomoka.

3. Iwapo thermalstat iliondolewa. Itapelekea feni zisifunguke kwa wakati pale inapotakiwa hivyo gari huweza kuchemsha.

4. Kuchoka kwa raba ya kifuniko cha rejeta. Maji yatavuja taratibu haswa presha inapokua kubwa na mwishowe gari inaweza chemsha.

5. Kutosetiwa vizuri kwa Timing Belt baada ya Overhaul hii inaweza sababishwa na fundi kutotumia kifaa kiitwacho Timing Light. (Ni moja ya sababu watu wanaogopa kununua gari iliyofunguliwa injini).

6. Kukatika kwa panga moja wapo la feni yako. Feni haitazunguka vizuri, na hii hutokea zaidi wale wanaopita katika madimbwi yenye vijiti ambavyo vikipita katika feni wakati inazunguka huweza pelekea kukata moja ya panga la feni.

7. Water Pump kuchoka.

8. Kutoboka kwa rejeta baada ya kuigonga katika mawe

9. Oil kidogo au kutoibadirisha kwa mda mrefu

MADHARA

1. Kupinda kwa Cylinder Head. Hii inaweza kukulazim kufanya matengenezo ya nusu injini iwapo joto kilizidi kiwango


2. Kupasuka kwa kuta za injini itakayopelekea kuvuja kwa oil na hivyo kukulazim kufanya matengenezo makubwa


3. Kunoki kwa injini. Baada ya piston kukosa oil ya kutosha joto hupanda sana na vyuma kuanza kusagana mwishowe unaweza kuua injini (Kukaanga mashine)

NB

Kila uwapo barabarani angalia dashboard yako kuhakiki mshale wa joto usivuke nusu


Jenga utamaduni wa kukagua gari yako mara kwa mara kwenye mfumo wa maji na oil.

Pia ni vuzuri kila unapomuazima ndugu au jamaa gari yako umuulize iwapo ameona tatizo lolote katika mfumo huo(si wote ni waaminifu kuweza kukwambia ukweli sababu ataogopa kuonekana mhalibifu).

Kwa ushauri tembelea ofisi zetu za Dar au Mbeya

IMG_20210526_105859_047.jpg
20210526_104742.jpg
 
Back
Top Bottom