Picha: Safari ya Kikosi cha Simba SC toka katika Fukwe za Bahari hadi kisiwani Unguja

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Mazoezi haya mithili ya special unit za Mossad yalianzia katika gym na fukwe za Jiji la Dar es Salaam, ambapo zoezi zima liliongozwa na kocha mwenye leseni ya juu kabisa toka UEFA ( Grade A) "Mtalamu" Dylan Kerr, akisaidiwa na moja ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika ardhi ya Tanzania, Seleman Matola.

View attachment 272305

View attachment 272307

View attachment 272309

View attachment 272312

View attachment 272314

Baada ya kazi ya wiki kadhaa, jeshi zima la Simba SC lilielekea Lushoto, kwa ajili ya mazoezi ya utimilifu mwili.. ambapo Kocha bora kabisa wa viungo mwenye heshima kubwa saaana nchini kwake(Serbia) Susan Momclovic, na huko mambo yalikua hivi;

View attachment 272319





Baada ya mazoezi hayo ya kijeshi.. Timu ilitua Zanzibar kwa ajili ya kujifua mbinu za uwanjani.. Na huko mambo yanaenda vizuri sana, kwani timu imeshakwiva.. Na anaeongoza hilo zoezi ni Kocha Mkuu Kerr, akisaidiwa na watalaamu wenzake.. Cheki picha chini hapo.









Mpaka sasa jeshi la maangamizi bado lipo Zanzibar, likimalizia malizia maandalizi yake kwa ajili ya msimu ujao.. Ndani ya siku mbili tatu, kikosi kizima kitatua kwa ajili ya kusherekea wiki ya Simba Day.

"Kwa kikosi hiki cha sasa, majirani zetu mjipange vyema, maana kuna hatari ile rekodi iliyowekwa na kile kikosi cha kina Kibaden ikavunjwa msimu ujao" - Sembo
 

Mkuu nafatilia kwa ukaribu sana tena sana na leo saa mbili usiku tuna game Amani stadium mashabiki wanaoitakia mema timu yetu mje kwa wingi sana pale amani tufanye kama tulichowafanya kombaini ya zanzibar Simba sc oyee NGUVU MOJA
 
Mkuu nafatilia kwa ukaribu sana tena sana na leo saa mbili usiku tuna game Amani stadium mashabiki wanaoitakia mema timu yetu mje kwa wingi sana pale amani tufanye kama tulichowafanya kombaini ya zanzibar Simba sc oyee NGUVU MOJA

Safi sana Mkuu.. Sasa hivi timu imeshaanza kuchanganya, naimani leo tutaibuka na ushindi mnene sana.
 
Waiteni wale wa mafurikoni waje huko zenji

Mkuu, wazee wa mafuriko sasa hivi wapo wanaomboleza msiba wa jana.. Hadi kukaa sawa najua ligi itakua ishaanza.. Na pia naona baadhi ya wachezaji wakifunguliwa mlango wa kutokea,
 
Safi sana Mkuu.. Sasa hivi timu imeshaanza kuchanganya, naimani leo tutaibuka na ushindi mnene sana.

Yaani kiongozi ile siku zilipigwa pasi uwanja wa amani wakawa wanaulizana ni simba hii au timu ipi baada ya kumuona ndemla kati akiwaunganisha vizuri kina simon serekuma mgosi malyanzi dah leo saa moja tu nipo uwanjani kushangilia chama langu tupo tayari kupeleka kilio tena jangwani msimu ukianza
 

Mkuu tunakutegemea sana kwa updates za soka la uhakika litakalotandazwa leo na Mnyama.
 

Unanitamanisha sana mkuu sijui niogelee hadi Zanzibar sasa hivi niiwahi hiyo mechi!
 
Mkuu tunakutegemea sana kwa updates za soka la uhakika litakalotandazwa leo na Mnyama.

samahani mkuu kwa kutoka kwenye mada, hawa kampuni ya jumia wameweka simu ambayo ni inactive najaribu kuwapigia ili nipate jezi simu haipatikani. wasitue watuwekee active namba tupate huduma hiyo
 
Mazoezi ya kuwa nafasi ya 4 hayo..!!Kelele nyingi mwisho wake ni 4th place.
 
Simba tuko mbele goli 3 -0

Mkuu wafungaji ni kina nani?! Ule msemo wa "hard work pay" ndo napoona ukifanya kazi yake.. Hongera Kerrr kwa kutubadilishia timu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…