Picha & taswira za yaliyojili kwenye mahakama ya Kisutu wakati Sheikh Ponda alipofikishwa Mahakamani

Picha & taswira za yaliyojili kwenye mahakama ya Kisutu wakati Sheikh Ponda alipofikishwa Mahakamani

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801



DSC_0502.jpg


Kiongozi wa Askari magereza, akiwaongoza Sheikh Ponda na wenzake, kutoka mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, baada ya kuahirishwa kwa kesi yao.


DSC_0473.jpg


Sheikh Ponda Issa Ponda, akifunguliwa pingu, baada ya kufikishwa kwenye chumba cha mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana Alhamisi Novemba 1, 2012.

Kiongozi huyo mwenye msimamo mkali, alifikishwa kwa mara ya pili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na wafuasi wake ambapo hakimu anayesikiliza kesi dhidi yake, Victoria Nongwa, ya kuvamia eneo la Markaz, Chang'ombe jijini Dar es Salaam, ambapo waliharibu na kuiba mali mbali mbali zenye thamani ya shilingi milioni 59, madai ambayo washtakiwa wote waliyakanusha.

Hakimu huyo alikubali kutoa dhamana kwa washtakiwa wote isipokuwa kiongozi huyo ambaye ni mshtakiwa namba 1 kwa madai kuwa bado Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), hajaondoa pingamizi lake la kuzuia dhamana kwa mshtakiwa namba moja.

Ulinzi katika mahakama hiyo ulikuwa ni mkali na haujawahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni, ambapo pamoja na mambo mengine, palifungwa CCTV Cameras, vifaa vya kugundua vitu vyenye asili ya chuma, polisi wa kutuliza ghasia magereza na wale wa FFU, polisi wa farasi na mbwa, pamoja na askari kanzu waliotapakaa kila kona ya maeneo ya jirani na mahakama hiyo kubwa jijini Dar es Salaam.

Kikundi kidogo cha wafuasi wa Sheikh Ponda, kilijaribu kuleta rabsha, lakini polisi walitumia busara na kuwaelekeza kilichoamuliwa mahakamani ambapo pamoja na kusuasua kuondoka eneo hilo la mahakama, lakini hatimaye waliondoka huku polisi wa kutuliza ghasia wakiwafuata kwa nyuma hadi eneo la makutano ya barabara za Bibi Titi na ile ya Morogoro nao wakatawanyika.

Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika vya habari, kulikuwepo taarifa kuwa wafuasi hao walipanga kutega milipuko kwenye eneo la mahakama na pia walisambaza vipeperushi vyenye vitisho kadhaa, ikiwa ni pamoja na kufanya maandamano makubwa ya kulazimisha kiongozi huyo aachiliwe.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena


Sheikh Ponda na pingu zake mikononi, akirejeshwa rumande.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Wafuasi wa Ponda, wanbaoshatakiwa pamoja naye, wakifunguliwa pingu mahakamani[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mshtakiwa akiwa amebebwa na mwenzake baada ya kudondoka mahakamani na kupoteza fahamu[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Askari wa kutuliza ghasia magereza, akiwa ameshika lindo mbele ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Alhamisi Novemba 1, 2012[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Polisi wa Mbwa nao walichukua nafasi yao[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Huiingii mahakama ya Kisutu bila ya kukaguliwa na mashine za kugundua vitu vya asili ya chuma hapo.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Farasi wa polisi wakiwafukuza wafuasi wachache wa Sheikh Ponda, waliojikusanya nje ya uzio wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Alhamisi Novemba 1, 2012[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Polisi wa Mbwa wakisubiri amri ndani ya gari lao nje ya mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Novemba 1, 2012[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Polisi wa Mbwa akifanya doria kwenye barabara ya Bitbi Titi mbele ya jengo la mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Askari Magereza wa kutuliza ghasia, aliyejihami kwa silaha na vifaa vingine akiwa makini kulinda usalama[/TD]
[/TR]
[/TABLE]




Imetumwa Na: Emmanuel Shilatu at 10:35 PM
 
niliwahi waambia huko nyuma kuwa, hawa wanaodhani serikali imelala wanajidanganya eti wengine wakasema we can do anything if we want, niliwambia fanyeni mtaona. Kama ni kasheshe za kisiasa hizo zinavumilika lkn zile za kutugawa kwa misingi ya kidini haikubaliki hata kidogo. SASA MMEONA MATENDO YA WALIOAPA KUILINDA KATIBA, PM kasema tutakuwa wakali kukabili hawa wakorofi wachache
 
Nikimuangalia Sheikh Ponda kwa umakini namuona kama mtu anayejuta kwa alilofanya na ni dhahiri amekata tamaa maana hakuna dalili yoyote ya maandamano tena ili atolewe.
 
Nina hofu sana na kinachozungumzwa na waislamu huku mtaani yaani
kama watafanya wanavyozungumza, Amani imekwisha na Dar haitakalika
Naomba Mungu niwahi kusafiri kabla hayajatokea hayo.
 
HAWA ASKARI wanao Vaa MAGWANDA MEUSI ndio WANAITWA NANI???
wanaitwa karibia na fujo zako ufe, jina lingine wanaitwa ifanyie fujo JMT au nchi ya JK ufe,
ndiyo maana wafuasi wa Ponda walipoona nembo za majina yao vifuani, ya karibia na fujo zako ufe, wakafyata mkia na kutokomea mitaani huku wakijichanganya na raia wema
 
Kulikuwa na sababu gani ya kutumia jeshi la JWTZ safari ile kutawanya maandamano wakati askari wa kutuliza ghasia wana full gear. Kama hao walovaa body armor sijawahi ona isipokuwa Tanzania na kwenye filamu za majeshi ya zamani ya wafalme
 
Umemtazama vibaya sana, yeye na wafuasi wake wanaonekana
kuwa na utulivu mkubwa na kuchukulia yanayotokea kama sehemu
ya Ibada.
Inawezekana Mkuu, labda mimi ndio nimemuangalia kwa huruma maana nimefikiria mambo mengi sana pia nikiwaza kuwa yeye anajisikiaje kuwa katika pingu zile pingu na kwanini hakufuata sheria kudai hicho kiwanja wanachogombea?
 
Ponda kapendeza kweli na zile pingu utafikili wamwache nazo ki1.
Halafu yule jamaa aliyeact kazimia du ameniacha hoi ?
Kazimia mikono imeficha uso ?
Mi nahisi kazi hamsini wala hajazi mia.
 
Nina hofu sana na kinachozungumzwa na waislamu huku mtaani yaani
kama watafanya wanavyozungumza, Amani imekwisha na Dar haitakalika
Naomba Mungu niwahi kusafiri kabla hayajatokea hayo.
Hebu tudokeze yanayosemwa. Humu JF hakuna anayekujua wewe, tuambie tu, utakuwa pia umevisaidia vyombo vya usalama kukabiliana nao.
 
hawa ni askari magereza wa kikosi maalum: wajibu wao ni pamoja na kupambana na ghasia ndani ya magereza yetu. Wanajulikana kama KM. Jamaa hawa wanafanana sana na FFU
 
Umemtazama vibaya sana, yeye na wafuasi wake wanaonekana
kuwa na utulivu mkubwa na kuchukulia yanayotokea kama sehemu
ya Ibada.

Sheikh una maana kuchochea na kufanya vurugu, na kukamatwa na kufikishwa mahakamani ni sehemu ya ibada?
 
pole zao maana kweli gerezani sio pakuchezea ninaimani hata wafuasi wake wameoja joto ya jiwe na wamejua serkali ipo
 
Unachezea Wana siasa wewe? Kweli wasiosoma ni chakula ya waliosoma.

Wamesaidia CCM kushinda na Kikwete. Leo hii wao wana ZIMIA mahakamani, mwenzo weekend inakuja anakwenda kupumzika kijijini kwake Msata kwenye hekalu.

Ona hata walivyovaa na ulinganishe na wenzao akina CCM Top family. PUMBAVU.

Wamewatumia na wameona wanaanza kuvuka mstari (kama Nigeria vile) na ghafla mambo yamegeuka.

Ponda3.jpg
 
Kwa kweli kwa niliyoyao pale kisutu leo sijui kama watathubutu kuandamana tena
 
Hilo janga linalofuata mungu pekee ndo anajua kitakachotokea.Ni wakati wa Waislamu kukaa chini na kuchukua maamuzi magumu uvumilivu ukizidi unainekana muoga
 
Back
Top Bottom