Huyo mtoto kwa umri wake ni ngumu kusema kafanana na hiyo njemba moja kwa moja.
Kuna uwezekano mkibwa akabadilika ama akawa na sura ha baba yake halisi au vinginevyo.
Kwa haraka haraka unaweza sema kafanana na hiyo njemba, ila ukichunguza sana utagundua zipo tofauti kadhaa, kwa mfano ukiuchunguza mdomo wa huyo mtoto ni sawa sawa na mdomo wa Mond, halafu anzia hapo hapo kwenye mdomo panda hadi puani eneo hilo linafanana kabisa na Mond, Chunguza macho yao hao wote watatu ni kama wanafanana hivi hivyo ni ngumu kusema mtoto karanda macho ya nani, lakini ukichunguza mashavu ya mtoto na hiyo njemba ni kama yametolewa photocopy, nenda kwenye paji la uso, huwezi kitofautisha kati ya mtoto na hiyo njemba, pua ya mtoto na hiyo njemba tofauti yake ni kwamba ya huyo njemba ni kubwa ila ya mtoto ni ndogo, kitu kingine ni kuhusu viini vya macho, hivyo viini vya macho ya mtoto ni kama vya Mond, angalia chunguza vizuri utabaini, jamaa viini vya macho yake ni vidogo vimeacha sehemu kubwa nyeupe ya jicho wakati Mond na mtoto wao viini vyao ni vikubwa vimeacha sehemu ndogo nyeupe ya jicho. Kitu pekee cha tofauti kwa mtoto huyo ni maoteo ya nywele ambayo si ya Mond wala hiyo njemba, maoteo ya nywele nadhani amechukua kwa mama yake Bi Zarina Hassani.
Nb: sehemu za uso alizofanana nazo mtoto na hiyo njemba kuna uwezekano mkubwa mtoto atakapofikisha umri fulani kubadilika wakati alizofanana na Mond haiwezekani.
Tuleteeni picha zinazoonesha sehemu za vidole vya miguu, vya mikono na masikio ili tupate ukweli, kufanana uso/rangi sio dalili ya kuchakachuliwa. Ogopa mwanao kufanana vidole vya miguu kama dole gumba, au masikio.