Picha: Uthibitisho Mwijaku kutumiwa na TTB kutangaza utalii

Kwani kuna ubaya!?,Mwijaku si ni raia wa Tanzania!?.., watanzania tuna matatizo sana. Mwenzetu mmoja akichomoza kuelekea kuWin tunaanza vita vya thread + picha😁
Uliona aibu anazozifanya huko lakini? Katika civilized world pale kwenye bus walikuwa wanamuona kama mental fulani. Hakuna impact kwenye utalii.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.Mwijaku alistahili pongezi badala ya kutaka kumchulia hatua.Amefanya kazi ya uzalendo kabisa ambayo board ya utalii wangewaza kumpatia cheti badala hiyo press release.Tanzania haijulikani kabisa Kwa watu wengi wa nchi za ulimwengu wa Kwanza.Najua kupitia yeye kuna wazungu ambao soon watakuja kutalii kupitia promo alizofanya.Board iache mihemuko kijana ametumia kipaji chake na uchangamfu wake kuiweka Tanzania kwenye ramani mnampa lawama...😁
 
Uliona aibu anazozifanya huko lakini? Katika civilized world pale kwenye bus walikuwa wanamuona kama mental fulani. Hakuna impact kwenye utalii.
Sijaziona aibu alizofanya, ziweke hapa tuzione tujadili kama ni aibu au mtazamo wako, mkileta thread weka taarifa kamili. Mleta uzi kaandika uthibitisho....., kidogo kaweka picha kama vile kila mtu anamfatilia Mwijaku masaa 24. All in all mtu yeyote ana haki ya kuitangaza Tanzania kwa namna anavyoona. Ili mradi asivunje sheria za alipo.
 
story siijui kiundani lakini ukipewa kazi kwa mkataba wa muda flani lets say mwaka kutangaza utalii mkataba ukaisha bado utakuwa mtangazaji wa utalii???

bongo zozo ni balozi wa utalii tanzania mkataba ukiisha akiendelea kutangaza utalii hapo hajatumwa na ttb.

nadhan TTB walichosema hawajamtuma mwijaki ufaransa. ila hawajamnyima kutangaza utalii FULLSTOP.
 
Kwani kuna ubaya!?,Mwijaku si ni raia wa Tanzania!?.., watanzania tuna matatizo sana. Mwenzetu mmoja akichomoza kuelekea kuWin tunaanza vita vya thread + picha😁
Ametumwa na nani,serikali ina njia zake zq kufanya kazi
 
Kwani kuna ubaya!?,Mwijaku si ni raia wa Tanzania!?.., watanzania tuna matatizo sana. Mwenzetu mmoja akichomoza kuelekea kuWin tunaanza vita vya thread + picha😁
me sijaona TTB walipokosea kutangaza utalii ni ruksa kwa kila mtanzania kwa mapenzi yako binafsi na Tasisi inawatu wake wakutangaza utalii kwa masharti yao na mipaka yao ya utangazaji.

mwijaki ninavyomjua atakuwa amevuka mipaka, kitu ambacho taasisi imeona itakuwa fedheha kwa bodi nzima ya TTB nje nchi kuwa na wajinga wanaotangaza biashara muhimu kama utalii.

mfanyakazi wa NMB akiiba hela ya mteja.
NMB bank ndo inapokea kashfa na sio mfanyakazi.
 
Uliona aibu anazozifanya huko lakini? Katika civilized world pale kwenye bus walikuwa wanamuona kama mental fulani. Hakuna impact kwenye utalii.
Sasa Aibu gani bana acheni ushamba yaani mtu kucheza mziki ndo Aibu.Acheni roho mbaya zenu nyeusi.
 
Mwijaku anadhani kutangaza utalii ni sawa na kuuza mitumba soko la Karume.??
Kelele nyingi + nguvu kubwa hadi boksa inavuja maji...
Aelewe utalii ni taaluma kama zilivyo nyingine.
Asirukie treni kwa mbele atagongwa nyuma.
 
Kutangaza utalii ni taaluma na sio comedy, na kujutangaza wewe ni balozi wakati unayoyafanya ni kituko, na mbaya zaidi TTB hawakukutuma lazima wakukatae mapema.
 
umemaliza kila kitu.
 
Ametumwa na nani,serikali ina njia zake zq kufanya kazi
Kwani kafanya nini kinyume na kanuni na sheria za nchi!?,mbona hamleti hapa alichofanya tofauti?,mleta mada kaandika uthibitisho....., uthibitisho wa nini!?,Mwijaku kakosea nini kuitangaza Tanzania!?, mbona watu wanaitangaza Tanzania kwa njia mbalimbali tena bila kutumwa na mtu au bodi yoyote, tatizo kwa Mwijaku ni lipi!?
 
Nani amemtuma kuitangaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…