PICHA: Wanafunzi wote wasinzia Darasani, nusu saa tu baada ya Mtihani kuanza

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
[TABLE="width: 782"]
[TR]
[TD][FONT=Georgia !important]06/11/2012[/FONT]



By Mohamedi Mtoi
[FONT=Georgia !important]

Picha zinawaonesha wanafunzi waliokuwa katika chumba cha darasa wakifanya mtihani wa Taifa wa kidato cha pili ulioanza jana nchini kote Tanzania.

Wanafunzi hawa walianza kusinzia mmoja mmoja ilipogonga nusu saa tu baada ya muda wa kuanza mtihani wa Hisabati ambao ulipangiwa saa mbili. Wanafunzi walionekana hoi huku wengi wakizikusanya karatasi zao za mitihani bila kuandika majibu ya maswali zaidi ya matatu.

wavuti.com inayo video inayoonesha wanafunzi karibu wote wakiwa wamesinzia, ila kwa sababu za kimaadili, video hiyo haitawekwa hapa ili kuwasitiri baadhi ya wanafunzi ambao sura zao zinaonekana dhahiri.

Ikiwa unataka maelezo ya ziada, tafadhali wasiliana na MohamediMtoi

[/FONT]













[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Source: Wanafunzi wote wasinzia darasani, nusu saa tu baada ya mtihani kuanza - wavuti.com
 

Sasa WAZIRI amesema kuwa MTIHANI wa MWAKA HUU watakaofeli watubaki FORM TWO; Hawata panda kwenda FORM THREE... Sasa hawa WAMELALA labda ni PRIVATE SCHOOL sidhani kama Wazazi watalipia MHULA MMOJA MARA MBILI

HALAFU wakifeli TENA ETI WANAFUKUZWA SHULE na watafanya kama PRIVATE CANDIDATE
 
Mi nilifkiri ni aw Shule zetu za kata tu! Nafkiri wangerusu huu mitihani uwe 45 minutes wanatuchosha wasimamizi YAANI wanalala tu
 
There might be something behind, this is not normal. There is a problem.
 
There might be something behind, this is not normal. There is a problem.

Hamna hata kitu ni normal kabisa we Leo ukipata chance tembelea Shule mbili tatu hivi especially za kata utaona kwa macho yako watoto wetu Sa hivi ni MATABULA RASA aka Mbulula hamna kitu KICHWANI na wastani wasipoushusha hadi 15 ni balaa majority watafeli
 
Mbona ni kawaida kabisa tena siku hizi hasa kwenye mtihani wa Mathematics.

Kwa hizo picha zilivyo inaashilia wamejilaza kwenye madawati kumaanisha kuboreka na kushindwa kwao kwenye mtihani na sio kulala usingizi au kusinzia.

Kuna kitu kinaitwa Mob Psychology, yaani wanawafunzi muhimu ''vipanga'' hata wawili wakiinamisha vichwa kwenye desk kuashilia kushindwa basi vilaza wote nao watafuata tu.

Vile vile wasimazi wa mitihani huwa wanaelekeza wanafunzi wanapomaliza mtihani kulaza vichwa chini kama ishara ya kupumzika, kumwomba Mungu au kupunguza usumbufu wakati wanasubiri muda rasmi wa kukusanya mitihani ufike.
 

Sikatai kwamba vilaza wapo, ila inawezekana darasa zima kulala darasani eti kisa namba haipandi kichwani? Hii kali.
 
Sikatai kwamba vilaza wapo, ila inawezekana darasa zima kulala darasani eti kisa namba haipandi kichwani? Hii kali.

mi ni msimamizi mkuu Jana after 30 minutes vyumba vyote vitano wanafunzi walikuwa doro na waliokuwa wanaandika walikuwa wana copy maswali
 
Hili jambo ni la kweli nasimamia shule moja ya binafsi ukiwapa mtihani tuu baada ya nusu saa zaidi ya nusu ya darasa wamelala mpaka masaa 2.30 yaishe na ni mitihani yote siyo hesabu tuu. Nitatizo la kizazi cha bongo fleva.watafeli wengi serikali itawapeba kwa maslai ya kisiasa. Wadanganyika sie.
 
Kama ni havo lbda mda waliopewa ni mrefu sana ukilinganisha na kiwango cha maswali
 

Sentensi yako ya mwisho sikubaliani nayo! Kama kweli ni wasomi hawawezi kusinzia darasani hata kama mtihani ni mrahisi na wamemaliza mapema huwa wanaruhusiwa kutoka baada ya muda fulani.
Hii ya kusinzia hasa ktk somo la hisabati ni ishara tosha kuwa hawaliwezi (hawataki) hilo somo.
Tuendako ni kugumu sana hata wakifukuzwa shule tatizo bado liko palepale. Dawa ni kubuni mkakati wa elimu utakaokubalika na kuendana na watoto ili wapende shule na wajifunze kwa bidii. Ni mbaya sana mtoto kufeli kwani inamkatisha tamaa, waalimu wapewe kipaumbele ili wafundishe watoto wote waelewe.
 
Ni normal shule za kata hamna kitu watoto wanakwenda kukua tu,so sad!!
 
Tunasubiri matokeo kwa hamu kubwa sanaaaa... Tunataka kufanya tathmini ya janga linalolikabili taifa. Jamii inapaswa kudhihirishiwa ya kwamba Tanzania is no more academically!
 
hata wakirudia mara10 kama walimu ni wawili hawa watoto wameandaliwa kufeli tu.. ni elimu gani ya walimu 2 secondary?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…