SI KWELI Picha ya anayedaiwa raia wa Afrika Kusini akichoma mahindi baada ya kuwafukuza wageni

SI KWELI Picha ya anayedaiwa raia wa Afrika Kusini akichoma mahindi baada ya kuwafukuza wageni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kumekuwepo Picha inayosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii ikimuonesha raia wa Afrika Kusini akichoma mahindi imezua mjadala mkubwa miongoni mwa watumiaji wa mitandao hiyo.

Katika machapisho mbalimbali yanayosambazwa mtandaoni, inadaiwa kuwa raia huyo wa Afrika Kusini amechukua kazi ambayo hapo awali ilikuwa ikifanywa na raia wa Zimbabwe.

Hata hivyo, je, madai hayo yana ukweli wowote? Uhalisia wa picha hiyo inayosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii ni upi?

Picha hiyo imechapishwa hapa, hapa hapa,
ZULU.jpg
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook na X kumekuwa na picha inayosamba ikumuonesha mwanume mmoja akichoma mahindi yaliyoungua na kudaiwa kuwa ni raia wa Afrika Kusini akifanya kazi walizowapokonya raia kutoka nje ya nchi yao ikiwemo Zimbabwe.

Madai haya pamoja na picha hii yameibuka kufuatia mgogoro wa muda mrefu ambao umekua ukiendelea nchini Afrika Kusini ambapo wenyeji wamekuwa wakiwatimua watu wasio raia wa nchi hiyo kwa kudai wanachukua kazi zao.

Uhalisia wa picha hiyo ni upi?

JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa picha hiyo si ya kweli bali imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde (AI).

Kwa kutumia nyenzo za kidigitali, zimeonesha kuwa picha hiyo imetengenezwa ama kuwa na viashira vya teknolojia ya Akili Unde kwa zaidi ya asilimia 50.
1781684978615-png.3609712

Picha-Uchambuzi wa sightengine

1781684997701-png.3609713
Picha-Uchambuzi wa hive moderation​

Picha hii inaweza kuwa imetengenzwa kwa lengo la kukosoa jambo fulani na ikiwa haitotolewa taarifa ya awali lengo la Taarifa hiyo inaweza kuhesabika pia kama upotoshaji.
Back
Top Bottom