Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
PICHA HII INAWEZA KUKUTOA MACHOZI
Dr. Salmin Amour aliyekuwa Rais wa Zanzibar alipotembelewa na Dr. Hussein Mwinyi nyumbani kwake.
Dr. Salmin kanyanyua mikono anamwelekea Allah kwa dua na dua siku zote ni kuomba kheri.
Dr. Salmin hivi sasa ni kipofu.
Haoni.
Amenyanyua mikono yake kamwelekea Allah anamuombea dua kijana wake ambae kama yeye miaka 25 iliyopita anasimama kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar katika hali ile ile ngumu na ya hatari kwa usalama wa visiwa wakati alipokuwa anamkabili Maalim Seif katika nafasi hiyo hiyo ambayo Dr. Hussein Mwinyi anaitaka na dhidi ya mtu huyo huyo na katika hali ya hatari ile ile iliyokabili Zanzibar mwaka wa 1995.
Msomaji wangu nakutaka radhi kwa sentensi ndefu nimeifanya hivyo kwa kusudi ili usivute pumzi wala kumeza mate katika msisitizo ulio ndani ya sentensi hii.
Dr. Salmin Amour alikuwa anaitwa Komando yaani mpiganaji hodari anaemudu kuzitumia silaha zote za kivita kwa ufanisi mkubwa mpiganaji ambae kifua chake kipana na mwenye misuli iliyotuna inayotisha adui.
Dr. Salmin Komando hotuba zake zilikuwa kali za kuogofya.
Leo hii sipendi kuzisikiliza hotuba za Komando kwani zinanitia simanzi kubwa wala sipendi kumwangalia popote picha zake zinapoletwa.
Hakika Kibeku alikuwa Ungo.
Wewe kijitu ukizisikia hotuba hizi lazima utatetemeka kwani wewe una nini cha kumtisha Komando?
Mabingwa wa kutengeneza filamu wa Hollywood wametengeneza movie, "David," kisa cha Mtume Daud.
Kuna kipande na Allah kakieleza kisa hiki ndani ya Qur'an pale Daud alipotoka kwenda kumkabili Jalut katika mapigano huku wote wakiangaliwa na majeshi yao.
Kisa Maarufu.
Hollywood katika ubingwa wao kipande hiki cha Daud anakwenda kupigana na Jalut wame-dramatise na kukuza kila kitu.
Kipande hiki kitakutoa machozi ukiwa utakiangalia huku unaileta ile dua ya Daud aliyokuwa anaisoma wakati anakwenda kupigana na Jalut akiwa hana silaha ila dua aliyofunzwa na Allah.
Jalut kasimama mbele yake jitu la miraba minne refu zaidi ya futi sita na kasheheni silaha nzito na deraya za chuma mwili mzima.
Maalim Seif alimshinda Komando katika uchaguzi ule na inasemekana Maalim ameshinda kila uchaguzi yaani kawashinda marais wote wa Zanzibar aliopambananao.
Dr. Salmin anaomba dua bila shaka ya kutafuta nusra Allah avinusuru visiwa na wananchi wake na shari iliyokuwa ishasimama ikisubiri cheche ndogo kulipuka.
Dr. Salmin anajua kinachomkabili Dr. Hussein Mwinyi kwani yeye kapita njia hiyo na anaijua vizuri kabisa.
Bila shaka katika dua hii yake Komando anamuomba Allah asijaalie Dr. Hussein Mwinyi akakalia kiti cha urais wa Zanzibar baada ya Wazanzibari kuuliwa.
Sote tunawajibu wa kunyanyua mikono yetu kuomba dua Allah ainusuru Zanzibar na shari ambayo tayari iko mlangoni.
Amin.