Picha ya Dkt. Salmin Amour na Dkt. Hussein Mwinyi inaliza

Picha ya Dkt. Salmin Amour na Dkt. Hussein Mwinyi inaliza

Kipindi hicho Ndio unaanza maisha maana mwaka 1980 Ndio ulikuwa na miaka 28 yaani kabwana kadogo kabisa, moh huwa unanifurahisha unavyusimulia matukio na watu waliokuzidi umri asiefahamu umri wako huenda akadhani wewe ni umri wakina Bomani au Butiku Kumbe hata 70 hujafika. Hongera
Makala...
Ahsante.
 
Connection ipo, Ndio maana tunaambiwa kufanya mema tukiwa na afya, muhali mtu atakae kuja dhoofu baada ya siha iliyombidiisha kufanya mema si sawa na alighulika na afya njema kwa kujivika kibri, Salmin amour angelikuwa hivyo umri wake wote sidhani kama angelikuwa na jeuri ile ya ukomandoo
Upofu unasababishwa na kutenda maovu?
Hayo maovu yana uhusiano gani na retina, iris, chochlea, knobs au chochote kwenye jicho.

Mimi nauliza uhusiano wa kibaiolojia sio hayo mambo yenu ya "angefanya mema angekuwa na afya". Kwani mtume alipoumwa alikuwa kafanya maovu gani. Ni wapi kwenye dini ulifundishwa mtu akiumwa/mlemavu chanzo ni maovu yake.
Watu waliozaliwa vipofu au walemavu maovu waliyatenda lini.
 
sio kuwa kipofu sasa hivi mavi popote sio unaona kuna debe hapo
 
Upofu unasababishwa na kutenda maovu?
Hayo maovu yana uhusiano gani na retina, iris, chochlea, knobs au chochote kwenye jicho.

Mimi nauliza uhusiano wa kibaiolojia sio hayo mambo yenu ya "angefanya mema angekuwa na afya". Kwani mtume alipoumwa alikuwa kafanya maovu gani. Ni wapi kwenye dini ulifundishwa mtu akiumwa/mlemavu chanzo ni maovu yake.
Watu waliozaliwa vipofu au walemavu maovu waliyatenda lini.
Upo upofu unaosabibishwa na maovu ewe mpendazoe na kwa sababu huelewi wacha nikutolee mfano wewe mwenyewe, huenda usingefikia hapo ingelikuwa ni muhanga wa uvamizi wa majeshi ya JWTZ
 
Upo upofu unaosabibishwa na maovu ewe mpendazoe na kwa sababu huelewi wacha nikutolee mfano wewe mwenyewe, huenda usingefikia hapo ingelikuwa ni muhanga wa uvamizi wa majeshi ya JWTZ
Sielewi kwa kuwa hakuna mnachoeleza. Eleza upofu unaosababishwa na maovu unatokeaje.
Kwenye causes of blindness kuna hiyo imani yako kama chanzo? Yani nimeomba maelezo mfano ''ukiua mtu, roho yake inatoka zinakuja kuganda kwenye lens ya jicho hivyo unakuwa kipofu". Nataka mfano kama huo kulingana na elimu yako.

Sasa nyinyi mnakuja na hadithi za kufikirika. Then, waliozaliwa vipofu walifanya uovu gani?
 
Tujitegemee,
Katika uchaguzi wa 1995 nilikuwa sehemu ya timu ya Prof. Lipumba na nilizunguka na yeye Bara na nilikuwapo Zanzibar siku ya uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi ilianza kubabaika pale siku ya pili asubuhi matokeo yalipoonyesha kuwa Dk. Salmin Amour ameshindwa.

Katika taharuki hii Ali Ameir akaandika barua ya kukataa matokeo.
Nakumbuka Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Ndugu Ali Amer akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani, Deutchvelee mchana ule wa Tarehe 24/10/1995
Alisema "....Uchaguzi umejaa kasoro nyingi na hujuma tele hasa kwa upande wa Pemba hivyo wao kama CCM hawatatambua matokeo yale na kuitaka tume ya uchaguzi ZEC kufuta na kurejea Uchaguzi..."

Ajabu siku mbili baadae 26/10/1995 Baada ya kutangazwa Komandoo kushinda kwa ushindi ule mwembamba wa kura 1500 na kura 4000 kuharibika Ndugu Ameir alibadili kauli yake huku akisema "tume ndio ina mamlaka ya mwisho na hivyo kutangazwa kwa Komandoo kushinda ndio uamuzi wa Tume na ndio wa mwisho"

Siasa za Zanzibar hazijawahi kuwa nyepesi kwa CCM tangu 1985.
 
SaSALMIN HAMJUI HUSSEIN MWINYI WALA HAMKUMBUKI NA PIA SALMINI HAONI SASA HAPO MWINYI ANAULIZWA NA SALMINI KWANI WW ULISOMA SHULE GANI HAPA ZANZIBAR MWINYI KAJIBU MM NIMESOMA MKURANGA NA NIMEZALIWA MKURANGA

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
PICHA HII INAWEZA KUKUTOA MACHOZI

Dr. Salmin Amour aliyekuwa Rais wa Zanzibar alipotembelewa na Dr. Hussein Mwinyi nyumbani kwake.

Dr. Salmin kanyanyua mikono anamwelekea Allah kwa dua na dua siku zote ni kuomba kheri.

Dr. Salmin hivi sasa ni kipofu.
Haoni.

Amenyanyua mikono yake kamwelekea Allah anamuombea dua kijana wake ambae kama yeye miaka 25 iliyopita anasimama kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar katika hali ile ile ngumu na ya hatari kwa usalama wa visiwa wakati alipokuwa anamkabili Maalim Seif katika nafasi hiyo hiyo ambayo Dr. Hussein Mwinyi anaitaka na dhidi ya mtu huyo huyo na katika hali ya hatari ile ile iliyokabili Zanzibar mwaka wa 1995.

Msomaji wangu nakutaka radhi kwa sentensi ndefu nimeifanya hivyo kwa kusudi ili usivute pumzi wala kumeza mate katika msisitizo ulio ndani ya sentensi hii.

Dr. Salmin Amour alikuwa anaitwa Komando yaani mpiganaji hodari anaemudu kuzitumia silaha zote za kivita kwa ufanisi mkubwa mpiganaji ambae kifua chake kipana na mwenye misuli iliyotuna inayotisha adui.

Dr. Salmin Komando hotuba zake zilikuwa kali za kuogofya.

Leo hii sipendi kuzisikiliza hotuba za Komando kwani zinanitia simanzi kubwa wala sipendi kumwangalia popote picha zake zinapoletwa.

Hakika Kibeku alikuwa Ungo.

Wewe kijitu ukizisikia hotuba hizi lazima utatetemeka kwani wewe una nini cha kumtisha Komando?

Mabingwa wa kutengeneza filamu wa Hollywood wametengeneza movie, "David," kisa cha Mtume Daud.

Kuna kipande na Allah kakieleza kisa hiki ndani ya Qur'an pale Daud alipotoka kwenda kumkabili Jalut katika mapigano huku wote wakiangaliwa na majeshi yao.

Kisa Maarufu.

Hollywood katika ubingwa wao kipande hiki cha Daud anakwenda kupigana na Jalut wame-dramatise na kukuza kila kitu.

Kipande hiki kitakutoa machozi ukiwa utakiangalia huku unaileta ile dua ya Daud aliyokuwa anaisoma wakati anakwenda kupigana na Jalut akiwa hana silaha ila dua aliyofunzwa na Allah.

Jalut kasimama mbele yake jitu la miraba minne refu zaidi ya futi sita na kasheheni silaha nzito na deraya za chuma mwili mzima.

Maalim Seif alimshinda Komando katika uchaguzi ule na inasemekana Maalim ameshinda kila uchaguzi yaani kawashinda marais wote wa Zanzibar aliopambananao.

Dr. Salmin anaomba dua bila shaka ya kutafuta nusra Allah avinusuru visiwa na wananchi wake na shari iliyokuwa ishasimama ikisubiri cheche ndogo kulipuka.

Dr. Salim anajua kinachomkabili Dr. Hussein Mwinyi kwani yeye kapita njia hiyo na anaijua vizuri kabisa.

Bila shaka katika dua hii yake Komando anamuomba Allah asijaalie Dr. Hussein Mwinyi akakalia kiti cha urais wa Zanzibar baada ya Wazanzibari kuuliwa.

Sote tunawajibu wa kunyanyua mikono yetu kuomba dua Allah ainusuru Zanzibar na shari ambayo tayari iko mlangoni.

Amin.View attachment 1566596
Nasikia WAPEMBA walipomlilia KOMANDO kuhusu kuonewa kwao aliwajibu

"MIMI SISIKII WALA SIONI" si unajua Wapemba tena na mambo yako ya kiswahili wakampa haja ya moyo wake leo HASIKII WALA HAONI
 
Ungo ukiwa mpya au mzima hutumika kwa kazi za vyakula kama kupepeta mchele au hata kuchagulia dagaa. Lakini ungo huohuo ukichakaa huitwa kibeku na hutumiwa kama zoleo la uchafu katika kufyagia uwanja.
Shukrani kwa kuniongezea nondo kali sana msamiati ila inaelekea "kibeku" pia ana umuhimu wake katika kufanya mazingira yawe safi ndio maana unaweza poteza muda kumtafuta ili kufanikisha zoezi.
 
Sielewi kwa kuwa hakuna mnachoeleza. Eleza upofu unaosababishwa na maovu unatokeaje.
Kwenye causes of blindness kuna hiyo imani yako kama chanzo? Yani nimeomba maelezo mfano ''ukiua mtu, roho yake inatoka zinakuja kuganda kwenye lens ya jicho hivyo unakuwa kipofu". Nataka mfano kama huo kulingana na elimu yako.

Sasa nyinyi mnakuja na hadithi za kufikirika. Then, waliozaliwa vipofu walifanya uovu gani?
sasa wewe toa elimu yako kwa nini kawa kipofu
 
Alikuwa na kauli chafu sana huyu jamaa enzi zake, lakini sasa si chochote si lolote. Be kind to the people on your way up because you will meet them on your way down.
Alikuwa mshenzi kwelikweli
 
Sheikh, hivi wakati wa kusoma DUA si huaga tunakaa kichini, mbona hawa masheikh wamekaa kwenye masofa tena? Au utaratibu umebadirika?
 
Sheikh, hivi wakati wa kusoma DUA si huaga tunakaa kichini, mbona hawa masheikh wamekaa kwenye masofa tena? Au utaratibu umebadirika?
umeyapata wap maelezo yako? du ainasomwa polpote na kwa sytle yoyote,au unaleta utan na dhihaka
 
Back
Top Bottom