lunatoc
JF-Expert Member
- Aug 16, 2017
- 2,911
- 5,479
Vipi unajisikiajeHawana timu,na kesho wanaokota mpira golini mara tatu
Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vipi unajisikiajeHawana timu,na kesho wanaokota mpira golini mara tatu
Hahaha pole kwa kipigo Cha Jana ...Cameroon afcon alikuwa anabebwa bebwa na marefa tu.
World cup anaanzia wapi kufuzu huku bara zima la africa lina nchi 60 zinagombea nafasi 5 tu.
mwarabu kamfunga cameroon akiwa kwake mechi ya kwanza. Sasa cameroon anaanzia wapi kwenda kupindua meza uarabuni.. kule anaenda kula 5 kwa bila
Wabongo mnajifanya wajuaji wa kila kitu Jana Algeria kafa 2-1 Tena nyumbani kwake.Song kocha wa timu ya taifa? jamaa hawako serious kabisa.
Hoja yangu wala haikuwa kufuzu kwenda world cup, ila performance yao kwa ujumla. Sijajua makundi yatakuwaje, ila akipata kundi lilichangamka hata draw sioni akiipata.Moira sio siasa nadhani huko uliko utakuwa unaumia Moyo kwa ulichoandika
Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
This thread didn't age well..Pole ndugu mchambuziPicha inaongea:
Wawili pichani ni wachezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, kulia ni Samwel Eto'o na kulia ni Rigobert Song.
Wakati wakicheza Samwel Eto'o alikuwa ni mchezaji tegemezi katika safu ya ushambuliaji na upachikaji mabao. Song yeye alikuwa mlinzi na ndiye alikuwa Kilanja au Nahodha(Captain) wa timu Yao ambayo si haba, ilikuwa na mafanikio ya kutosha ikitwaa mataji ya Afcon na kushiriki michuano ile mikubwa kabisa ya Kombe la Dunia.
Kwa sasa baada ya kustaafu kucheza soka, Song yeye ni kocha(mwalimu wa Mpira wa miguu), na Eto'o yeye kwa sasa ndiye Bosi wa Soka nchini Cameroon akiwa ndiye Rais wa chama cha soka cha nchi hiyo ya Afrika ya magharibi.
Kwa Imani aliyokuwa nayo kwa Captain wake wa zamani, Eto'o aliamua na kubariki kumkabidhi Song jukumu la kufundisha timu ya taifa, tena wakati ikiwa na ratiba ngumu ya kucheza michezo ya hatua ya makundi kupata tiketi ya kushiriki kombe la Dunia.
Pichani kama unavyoona, Eto'o akimuangalia kwa hasira Kocha wake mteule wa timu ya taifa baada ya Cameroon kupoteza Mchezo muhimu na mgumu katika uwanja wa nyumbani kwa bao moja kwa bila dhidi ya Timu ngumu ya Algeria.
Hakuna amani kati Yao, sura zao zinaongea, Eto'o akikunja sura kimamlaka na katika namna ya kulaumu, wakati Song yeye akiinamisha uso chini ishara ya kukiri au kujutia makosa.
Kuna kosa Eto'o amelifanya, ndio linalomgharimu, na kwa kiasi fulani anajutia kwa maamuzi yake ya kumwamini Kaka yake(kiumri) Song.
Majuto aliyo nayo Sasa hayawezi kubadili hali ya mambo, tayari wameshapoteza point Tatu, tena katika ardhi ya nyumbani, ni kosa kubwa sana kwa Mpira wa kileo ambao unalazimisha kila mtu kuhakikisha anashinda uwanja wa nyumbani.
Kosa alilofanya Eto'o ndiyo makosa ambayo wa Afrika wengi tumekuwa tukiyafanya na kutugharimu, kumwamini mtu kwa kuwa unamjua si kwa kuwa ana Vigezo.
Kwanini Eto'o alikubali kuifanya timu ya taifa kama field(darasa la mafunzo) kwa Song ambaye Nina uhakika hajawahi au hana rekodi yoyote ya kufundisha soka kwa mafanikio popote, iweje akaaminiwa kwa timu ya taifa?
Yaani ni sawa na hapa kwetu leo umpe majukumu ya Timu ya taifa Mecky Mexime au Mwanamtwa Kihwelu. Yes ni makocha wazuri na tutajivunia sana kama wako fanya vizuri, wakiharibu hatutokuelewa, na ni hapo wachambuzi wetu utawajua ni wachambuzi au wachang'ombe[emoji1787]
Lakini Kwa upande wa pili inawezekana kwa Imani ya Eto'o kwa wachezaji wa kizazi cha Sasa cha Cameroon aliona hakuna wa kuwazuia, akaona ni heri sifa za kufanya vema ziende kwa mzawa kuliko kwenda kwa mzungu.
Inawezekana yeye Eto'o anaamini sana kwa uwezo wa wachezaji uwanjani kuliko uwezo wa kocha kuwaunganisha wachezaji kimfumo.
Lakini kama dhamira yake Eto'o ilikuwa ni kuondoka utegemezi kwa makocha wa kigeni basi nampongeza kwa ujasiri na uthubutu wake.
Na kama aliamini katika MAZOEA kwamba Cameroon kwa kushiriki World Cup haina mjadala, basi anapaswa kuwaomba radhi wana wa Cameroon na Afrika kwa ujumla.
Lakini yote kwa yote, hii ya udugu (nepotism) na kujuana tukaacha weledi (professionalism) ndivyo vinaharibu Mpira WETU Africa.
'the Bridge is too far' Safari bado ni ndefu sana.
View attachment 2166977
Rudi huku uandike tena, muwage wavumilivuCameroon afcon alikuwa anabebwa bebwa na marefa tu.
World cup anaanzia wapi kufuzu huku bara zima la africa lina nchi 60 zinagombea nafasi 5 tu.
mwarabu kamfunga cameroon akiwa kwake mechi ya kwanza. Sasa cameroon anaanzia wapi kwenda kupindua meza uarabuni.. kule anaenda kula 5 kwa bila
Hata afrika tukipewa nafasi sabini tunaweza wabongo tusiwemo. Mtu akibisha muulize kimsimamo tupo wangapi.Wabongo tumejawa na ujinga sana, watu na akili zao fupi wanawaza hapa tu.
Sijui kama wanafahamu World Cup ijayo Africa itapeleka nchi 9 na ukiongeza nafasi moja ya play-offs tukawa na timu 10, ila usishangae bongo kutokuwa mmoja wapo!
Mmeanza tenaHoja yangu wala haikuwa kufuzu kwenda world cup, ila performance yao kwa ujumla. Sijajua makundi yatakuwaje, ila akipata kundi lilichangamka hata draw sioni akiipata.
Wamepelekwa na bahati sio kocha.Matokeo vipi
Mmeanza!!Wamepelekwa na bahati sio kocha.
Wandugu ebu tuwe tunafuatilia basi Mpira sio kushabikia tu, kwa mechi hiyo moja iliyomvusha kwenda WC haiondoi ukweli kwamba jamaa timu yao kwa sasa haipo sawa, na ushahidi ni ile performance yao mbaya kabisa kwenye afcon.Hoja yangu wala haikuwa kufuzu kwenda world cup, ila performance yao kwa ujumla. Sijajua makundi yatakuwaje, ila akipata kundi lilichangamka hata draw sioni akiipata.
Nakubaliana na wewe na ndio ilikuwa hoja yangu. Kwa kuanzia Algeria mwenyewe wala hakufanya vizuri kwenye Afcon hivyo hivyo hata kutolewa na Cameroon siyo kwamba Cameroon kapona "ugonjwa" uliokuwa unamsumbua.Wandugu ebu tuwe tunafuatilia basi Mpira sio kushabikia tu, kwa mechi hiyo moja iliyomvusha kwenda WC haiondoi ukweli kwamba jamaa timu yao kwa sasa haipo sawa, na ushahidi ni ile performance yao mbaya kabisa kwenye afcon.
Kumfunga Algeria Brothers nawaambieni sio ishu hata sisi Tanzania tushawahi Kumfunga huyo Algeria.
Kwa Cameroon ni vile tu wachezaji waliamua kuifia timu kwenye mechi ile.
Huyo ndio anaitwa mtu wa tatu wapo wengi sana hapa bongoKuna mwamba hapo pembeni anacheeka nahis moyoni anasema tulikuambia mh Rais lakn hukutaka kusikia
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Song ni mzee wa kupuliza na kuvuta ndum aka bangi anapewaje timu ya Taifa?Song kocha wa timu ya taifa? jamaa hawako serious kabisa.