KWELI Picha ya Ibrahim Traoré akiwa amevalia kofia yenye bunduki imehaririwa kwa kutumia akili unde

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kumekuwepo na picha inayosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram na X ikimuonesha Rais wa Burkina Faso, Ibrahim Traoré, akiwa amevalia kofia nyekundu ambayo inaonekana kuunganishwa moja kwa moja na bunduki.

Hata hivyo, uchunguzi wa kidijitali umebaini kuwa picha hiyo imehaririwa kutoka kwenye picha halisi na kufanyiwa maboresho kwa kutumia teknolojia ya akili unde , jambo linaloifanya ionekane tofauti na uhalisia wake wa awali.

Aidha, ufuatiliaji zaidi umeonesha kuwa picha hiyo inayosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii haijawahi kuchapishwa na vyombo vikubwa vya habari nchini Burkina Faso wala kutolewa kupitia vyanzo rasmi vya serikali, jambo linaloibua mashaka makubwa kuhusu uhalisia wake.

Kutokana na ushahidi huo, inaonekana wazi kuwa picha hiyo si halisi bali ni picha iliyohaririwa kwa lengo la kuvutia hisia za watu na kuongeza usambazaji wake mtandaoni.
683583551_1404862431687296_8427770376875096663_n.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na picha inayosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram na X ikimuonesha Rais wa Burkina Faso, Ibrahim Traoré, akiwa amevalia kofia nyekundu ambayo inaonekana kuunganishwa moja kwa moja na bunduki.

Hata hivyo, uchunguzi wa kidijitali umebaini kuwa picha hiyo imehaririwa kutoka kwenye picha halisi na kufanyiwa maboresho kwa kutumia teknolojia ya akili unde , jambo linaloifanya ionekane tofauti na uhalisia wake wa awali.

Picha halisi ilichapishwa mtandaoni kuanzia mwaka 2024 ambapo vyanzo mbalimbali viliichapisha taarifa zao vikiambatana na picha hiyo, mathalani BBC na VOA waliitumia picha hiyo katika makala zao mwaka 2024 na 2025.
1777451078982-png.3581268

Picha halisi, Chanzo Reuters​

Back
Top Bottom