SI KWELI PreGE2025 Picha ya magari aina ya Ford Ranger yalioandikwa CHAUMA yawasili nchini

SI KWELI PreGE2025 Picha ya magari aina ya Ford Ranger yalioandikwa CHAUMA yawasili nchini

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
1747832397315.png

1747126094222.png
 
Tunachokijua
Akili mnemba (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.

Ujio wa teknolojia hii umeathiri kwa kiwango kikubwa mfumo wa utengenezaji na usambazaji wa taarifa kwani inampa mtumiaji uwezo wa kutengeneza maaudhui katika muundo wa picha, video, maandishi ama sauti kwa ubora wa hali ya juu ambapo wakati mwingine yanaweza kutumika kwa lengo la kupotosha.

Na Kama ilivyo kwa maeneo mengine ulimwenguni Tanzania pia inakumbana na kadhia ya maudhui ya upotoshaji yanayotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba hivyo ni muhimu sana kufahamu na kujifunza kila wakati mbinu zitakazokuwezesha kutambua maudhui yaliyotengenezwa kwa teknolojia hiyo ili kuepuka upotoshaji unaoweza kufanyika katika sekta zote za jamii.

Ipo picha ambayo imekuwa ikisambazwa mtandaoni ikidaiwa kuwa ni magari yaliyowasili nchini kwa ajili ya chama cha siasa CHAUMMA.


Je, picha hiyo ni halisi au imepotoshwa?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa picha hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba.

Vile vile picha ina mapungufu ambayo yanakinzana na uhalisia. Uwepo wa mashine ambayo inatumika kushushia makontena ambayo sehemu ya nguzo zake zinaonekana kuingia ndani ya meli jambo ambalo si la kawaida.
1747134384584-png.3332588


Pia magari yamebainika kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo kutokuandikwa kwa usahihi kwa jina la gari ambalo ni 'FORD' huku magari mengine yakiwa hayaoneshi kutenganishwa kati ya mlango wa mbele na nyuma (zingatia gari ya kwanza)

Tofauti na ilivyoandikwa katika magari hayo chama hicho jina lake rasmi huandikwa 'CHAUMMA' na si 'CHAUMA'

Hata hivyo kifaa cha utambuzi wa madhui yaliyotengenezwa kwa akili mnemba kinabainisha kuwa upo uwezekano wa asilimia 52 wa picha kutengenezwa kwa teknolojia hiyo.​
Hii chart gtp unatakiwa kupigwa marufuku ..lakini hata Mimi inanisaidia hapa kijijini kwangu wananisifu...mf..MTU anakuja anataka kumpa notise mpangaji wake chini ya dk 2 nakuwa nishamprintia document yake au MTU anakuja Ana malalamiko Fulani kwenda kwa kiongozi Fulani chini ya dk unakuwa ushapata content
 
Back
Top Bottom