Picha ya Makatibu wa Kwanza Tanganyika Baada ya Jamuhuri 1962

Picha ya Makatibu wa Kwanza Tanganyika Baada ya Jamuhuri 1962

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,526
Reaction score
34,057
1779034124916.png

Hii ni picha ya makatibu wa kwanza baada ya nchi yetu kuwa jamhuri mwaka1962.

Katika picha hii walikuwa wamebaki watatu waliohai kabla ya kufariki dunia Paul Sozigwa aliye wa pili kulia msitari wa pili.

Tunao waombea mmaisha zaidi ni fredrick mchauru 97yrs aliye wa pili kushoto mstari wa pili pamoja na cleopa msuya aliye katikati mstari wa pili.

Mungu ampe raha ya milele paul sozigwa mwandishi wa kwanza kutangaza ziara za nje za mwal nyerere!
Amina

Utangulizi

Kuna Makatibu Wakuu watatu katika picha: Michael Lukumbuzya, Iddi Mwajasho na Fredrick Mchauru nina historia zao wakati wa joto la kupambana na ukoloni wa Muingereza lilipoanza.

Naanza na historia ya Michael Lukumbuzya:

Napenda nieleze mambo yalivyokuwa wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kipindi hicho ni cha TAA TANU bado haijaasisiwa.

Historia hii inamuhusu Chief Michael Lukumbuzya, Hamza Mwapachu na Abdulwahid Sykes na aliyenihadithia ni Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina Mama Daisy, mke wa Abdul Sykes.

Ilikuwa mwaka wa 1950 au 1951Gavana Edward Francis Twining amewaondoa Dar es Salaam viongozi wote wakuu wa TAA kwa kuwa walikuwa wanajihusisha na siasa.

Serikali ikatoa Government Circular kama onyo kwa watumishi wa serikali ya Mfalme George wajiweke mbali na siasa.

Dr. Vedasto Kyaruzi Rais wa TAA akatupwa Nzega, Hamza Kibwana Mwapachu mjumbe wa TAA Political Subcommittee akapelekwa kisiwani Nansio, Ukerewe.

Harakati zote TAA HQ New Street zikasimama pale kabakia Abdul Sykes Katibu wa TAA na mdogo wake Ally na wajumbe wengine kama Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Said Chaurembo.

Abdul Sykes akafunga safari na mkewe Mama Daisy kwenda Nansio kwa Hamza Mwapachu kutafuta ushauri nini kifanyike kukihuisha chama.

Hamza Mwapachu alimtayarishia Abdul Sykes mapokezi makubwa bandarini Nansio.

Zikapigwa ngoma za kienyeji kupokea Abdul Sykes TAA Act. President na Secretary.

Kwenye meli ile iliyotia nanga pale bandarini alikuwapo Chief Michael Lukumbuzya anarudi likizo kwao akitokea Makerere College, Uganda.

Lukumbuzya kapigwa na bumbuazi kashangaa anajiuliza huyu kijana mtanashati anaepokelewa na magoma ya wenyeji wa Ukerewe ni nani?

Hamza Mwapachu alimshauri Abdul Sykes TAA iajiiri Executive Secretary ili awe ofisini muda wote kuendesha shuguli za TAA.

TAA ikamuajiri Alexander Tobias.
Huyu akajakuwa kachero wa Special Branch ndani ya TAA akitoa siri zote za chama kwa Gavana Twining.

Historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU Ina mengi sana yasiyofahamika.
 
Back
Top Bottom