- Source #1
- View Source #1
Wakuu
Nimekutana na hii taarifa imenisikitisha sana. Inasema mama mwenye mtoto mdogo amedondoka ghafla mbezi na anahitaji msaada wa haraka.
JamiiCheck tusaidieni kuthibitisha taarifa hii, inaumiza sana.
Nimekutana na hii taarifa imenisikitisha sana. Inasema mama mwenye mtoto mdogo amedondoka ghafla mbezi na anahitaji msaada wa haraka.
JamiiCheck tusaidieni kuthibitisha taarifa hii, inaumiza sana.
- Tunachokijua
- "Leo asubuhi uko mbezi dada huyu aliyekua anauza uji uku akiwa na mtoto mchanga mgongoni ameanguka ghafra na kupoteza fahamu. Tumemkimbiza hospitali ya Mlonganzila mpaka Sasa Bado hajazinduka yupo ICU. Nimeposti hii hili kama Kuna mtu anamfahamu huyu dada awatarifu ndugu zake waje wamchukue mtoto na yeye apate uangalizi. Tafadhali kama una roho ya kibinadamu share au sambaza picha hii ili ndugu wapatikane waweze kumnusuru kwanza huyu mtoto mdogo asiye na hatia"
Ni ujumbe unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ukiambatana na picha ya tukio hilo, linalodaiwa kutokea Mbezi, ambapo mhusika anadaiwa kuwepo ICU akipatiwa matibabu, huku akiwa hajitambui.
Bila shaka, taarifa hii inagusa moyo na hisia za watu, kuithibitisha ili tufahamu uhalisia wake ni suala lenye uzito mkubwa.
Taarifa hii ina ukweli kiasi gani?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umebaini mambo yafuatayo:
1. Ni Taarifa ya Zamani
Marejeo ya Kimtandao kwa kutumia nyenzo ya Google Reverse Image unaonesha tukio halisi la picha hii lilitokea nchini Nigeria miaka michache iliyopita, ambapo baadhi ya kumbukumbu za kimtandao zinaonesha kuchapishwa kwake mwaka 2024.
Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi inayoelezea mhusika wa tukio hilo ni nani, alipatwa na nini na kipi kilisababisha adondoke.
2. Halijatokea Tanzania
Kama tulivyobainisha hapo juu, tukio hili lilitokea Nchini Nigeria.
Picha za uthibitisho zaidi zipo hapa.
3. Mkanganyiko wa Taarifa
Ufuatiliaji zaidi wa JamiiCheck umebaini taarifa hii imekuwa ikibadilika mara kwa mara. Mathalani, jioni ya siku hiyo hiyo, Februari 8, 2026, taarifa yenye maelezo hayahaya ilisambaa kwenye baadhi ya Mitandao ya kijamii ikidai aliyeanguka ni kijana wa kiume, muuza maandazi.
Wakati huu, eneo lililotajwa lilikuwa Kimara Mwisho.
Hii inaleta mashaka zaidi juu ya uhalali, usahihi na muktadha sahihi wa taarifa hii.
4. Uhalisia kutoka Mbezi na Kimara Mwisho
Baada ya kutumia nyenzo za kidigitali kuthibitisha taarifa hii, JamiiCheck ilifuatilia pia uhalisia wa taarifa hii kutoka sehemu zilizotajwa kuwa imetokea.
Kwa kimara Mwisho, taarifa za uhakika ambazo JamiiCheck imezithibitisha ni kuwa tukio hili halijatokea kabisa maeneo hayo, hivyo ni dhahiri kuwa ni tukio la kubuni, lisilokuwepo, lililotumia muktadha wa picha ya tukio la Nigeria.
Kwa Mbezi, hakuna taarifa yoyote ya kuaminika inayothibitisha kutokea kwa tukio hili.
Msimamo wa JamiiCheck
Tukio hili ni la kweli lakini halijatokea Tanzania kama inavyodaiwa.
Lilitokea nchini Nigeria, na kumbukumbu za kimtandao zinaonesha lilichapishwa mtandaoni Machi 4, 2025.
Rejea hapa kwa uthibitisho zaidi.