Kama sikosei hii ilikuwa ni mwaka 2005 baada ya uchaguzi uliomtangaza jk kuwa mshindi wa nafasi ya urais. Kwa ujumla, Chadema waliridhika na kuridhia matokeo na hapo kwenye picha inaonekana Kamanda Freeman Mbowe
akimpongeza jk bila kinyongo. Sasa kutokana na picha na maelezo haya, tunaweza kujifunza kwamba uchaguzi wa 2005 ulikuwa huru na wa haki na chadema waliridhika nao. Sasa basi, kama chadema ni chama kilekile na Mbowe, Dr. Slaa (PhD) na viongozi wengine ni walewale, kwa nini leo hii wasishikane mikono na jk? Ukweli ni kwamba uchaguzi wa mwaka huu haukuwa wa huru na wa haki.
Pia, picha hii inaonyesha umakini wa chadema katika kuendesha siasa za nchi hii na ni chama chenye msimamo thabiti wa kusimamia maamuzi yake. Hakina substandards katika kufanya mambo yake. Hongera viongozi wa chadema, wananchi tuna imani nanyi.