Picha ya Mbowe walipokutana na JK: Je unajifunza nini kwenye picha hii?

Picha ya Mbowe walipokutana na JK: Je unajifunza nini kwenye picha hii?

Kama sikosei hii ilikuwa ni mwaka 2005 baada ya uchaguzi uliomtangaza jk kuwa mshindi wa nafasi ya urais. Kwa ujumla, Chadema waliridhika na kuridhia matokeo na hapo kwenye picha inaonekana Kamanda Freeman Mbowe
akimpongeza jk bila kinyongo. Sasa kutokana na picha na maelezo haya, tunaweza kujifunza kwamba uchaguzi wa 2005 ulikuwa huru na wa haki na chadema waliridhika nao. Sasa basi, kama chadema ni chama kilekile na Mbowe, Dr. Slaa (PhD) na viongozi wengine ni walewale, kwa nini leo hii wasishikane mikono na jk? Ukweli ni kwamba uchaguzi wa mwaka huu haukuwa wa huru na wa haki.

Pia, picha hii inaonyesha umakini wa chadema katika kuendesha siasa za nchi hii na ni chama chenye msimamo thabiti wa kusimamia maamuzi yake. Hakina substandards katika kufanya mambo yake. Hongera viongozi wa chadema, wananchi tuna imani nanyi.



Gosbertgoodluck,

FYI: hii imetokea leo kwenye sherehe za kuadhimisha siku ya sheria nchini katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
 
Najifunza kwamba JK aliwahi kuingia Bilicanas disco kabla hajawa rais, akanywa akashindwa kulipa deni. Sasa anapoona Mbowe anamshika mkono kwa nguvu hivyo anaogopa asije akamkumbushia lile deni hadharani. (hehehe, joke)

Lakini, seriously, JK anaonekana kama anataka kujitoa akimbie. Hebu angalia hiyo picha vizuri. Inaonekana ile advetaizi ya Mbowe ya Arusha ilimtisha hadi leo!!!
 
Kwani mnatakaje? Wapigane? The bigger man is showing that his motives are peaceful. Iwe politics au la.
 
tanzania ilikiwa kabla ya cdm na ccm , vyama ni vyombo vya vitapita maisha yanaendelea
 
Wewe unadhani wanaongelea nini hapo?

Hapo Mbowe anamwambia "Mzee lakini na wewe kwa kuchakachua ni noma!"
Mkwere akajibu " Heri lawama kuliko hasara, Ulitaka niaibike"
Wote wakacheka "teh teh teh teh"
Hiyo ndiyo SIASA!
 
Mods nao naona wanaleta mambo ya censorship.. This is an issue of political significance albeit minor. THread imeletwa huku ili watu wasionie.. NDIO JF-CHADEMA hii... tukiwapa nchi mta tufanyia censorship. This is why I hate F@kn radicals... They all end up like Mubarak.

You are right man. I am pro-Chadema lakini nashangaa issue nyingine kunakuwa na uwoga wa kuogopa hata kivuli. Its just a photo guys! Lazima tuwe open.. Siasa sio vita.
 
Siasa ni sanaa km sanaa nyingine za uigizaji...si km muziki wa Hip hop ambao bila sababu ya msingi vijana wananuniana tu kisa ni kuwa shabiki wa kundi tofauti!...Mr Mbowe huo ndio ukomavu!
 
Jamani hii imekaaje? Nimeipata asubuhi hii kwenye StarTv kipindi cha Watanzania tuzungumze magazeti.
 
Kweli wewe sijui ni kuchambue vipi maana hata la kusema sina. Pole sana unategemea hii news unategemea itatoka Chadema, katika kuish kwako Tanzania inaelekea hujui siasa nini?
 
Ndugu Zangu,

JANA tumeona picha ya pamoja; JK akiwa na Freeman Mbowe.
Katika sanaa ya picha inasemwa, kuwa picha moja yaweza kuwa sawa na maneno elfu moja. Picha moja yaweza kutoa tafsiri nyingi.

Nimeitafakari picha ile. Ni moja ya picha nzuri iliyobeba ujumbe muhimu kwa Watanzania hususan tukikumbuka Uchaguzi uliopita na matukio baada ya uchaguzi.

Ni picha inayobeba matumaini badala ya kukatisha tamaa.

Inaonyesha, kuwa hata baada ya uchaguzi, maisha ya kisiasa hayana budi kuendelea. Na siasa si ugomvi. Siasa ni jambo jema. Ni wakati sasa kwa akina Freeman Mbowe na wenzake wa CHADEMA kuvua magwanda yale ya khaki na kushiriki maisha ya kawaida ya kisiasa.

Kama ningewashauri CHADEMA, basi, ningewaambia, kuwa , kwa kiongozi, vazi pia hutuma ujumbe kwa unaowaongoza. Magwanda yale ya CHADEMA yamekaa kijeshi zaidi. Labda yalitosha kuyatumia katika ' mapambano' ya kampeni za uchaguzi, lakini si sasa. Uchaguzi umeshapita.

Huu ni wakati wa kurekebisha tofauti zilizojitokeza na kwenda mbele. Na tuna cha kujifunza kutoka Unguja. Itakumbukwa, kuwa baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005, Maalim Seif alikaririwa akitamka kuwa; "Hakuna tena mufaka wa tatu". Rais Karume naye akakaririwa akitamka; "Sitaki kusikia habari ya Serikali ya mseto". Haya , leo Maalim Seif yumo ndani ya Serikali ya Mseto!

Na hapa kwetu CHADEMA walianza na kauli za kutoitambua Serikali. Nitakuwa mtu wa mwisho kushangaa siku ile Dr Slaa na JK watakapokaa meza moja na kongea kirafiki. Na tunaamini katika mazungumzo kama njia ya kutatua migogoro yetu ya kisiasa.

Kupitia picha ile ya jana tumeona busara za Rais Jakaya Kikwete, kusimama na kuongea na Freeman Mbowe katika hali ya kirafiki. JK ameonyesha kujiamini na kuendelea na kazi ya kuifatuta suluhu ya migogoro ya ndani ya nchi.

Kwa kiongozi wa kisiasa kuitafuta suluhu si udhaifu, ni ujasiri. Na huo ndio ukomavu wa kisiasa pia. Naamini, ndani ya CCM kuna wanaoogopa kupiga picha wakiwa pamoja na viongozi wa CHADEMA. Ni kwa kuhofia kuandamwa na wenzao ndani ya chama.

Tumefika mahali tukubali, kuwa siasa si uadui. Profesa wa Sayansi ya Siasa , Robert Dahl alipata kuandika;" Ni wajibu wa dola kuendesha juhudi za kutafuta suluhu za migogoro ya kijamii. Siasa ni hatua za majadiliano endelevu yenye kuhakikisha migogoro inapatiwa ufumbuzi kwa njia za amani". ( Theory and Methods of Political Science Uk. 211)

Tofauti za kifikra na kimitazamo ni mambo ya kawaida katika siasa. Kunahitajika majadiliano endelevu katika kupata ufumbuzi wa migogoro. Si lazima papatikane mshindi katika kila mgogoro, wakati mwingine hutengenezwa mazingira ya pande zote mbili kushinda, kila mmoja kujisikia ameshinda, a win- win situation.

Kwa sasa CHADEMA iukubali ukweli, kuwa Uchaguzi uliopita umeshapita. Kwamba Serikali iliyo madarakani kwa sasa ndio hiyo inayoongozwa na JK kama Rais. Hatuna Rais mwingine. Hatuna Serikali nyingine.

Na CCM nayo iukubali ukweli, kuwa wakati umebadilika na kuwa wananchi wanaukubali upinzani. Na kwamba kwa sasa, CHADEMA ndio chama kikuu cha upinzani kikifuatiwa na CUF.
Vyama hivi na vingine vyenye uwakilishi bungeni, vina lazima ya kushirikiana katika mambo ya msingi na yenye maslahi kwa taifa letu.

Tuache kujichimbia kwenye mahandaki. Tuanze sasa kuijenga nchi yetu kwa pamoja. Hatuwezi kuijenga nchi yetu katika hali ya vurugu , uhasama na chuki. Hii ni nchi yetu. Ni nyumba yetu tunayoijenga. Kwanini tugombanie fito?


Maggid
Dar es Salaam
Februari 3, 2011
 
Ni miezi kadhaa imepita tangu CHADEMA wakatae kumtambua JK kama raisi halali wa Tz, leo tunaambiwa kwamba mwnkt wa chadema Freeman Mbowe kamtambua JK kama raisi halali wa Tz, najiuliza ni kipi kimefanyika kudhibitisha uhalali wa huyu Mheshimiwa na wakamtambua? Kwangu mimi huu ni undumilakuwili na ukengeukaji! Haiwezekani ukawa mtu kigeugeu namna hiyo. Bwana Mbowe itabidi awashawishi wenzake nao wamtambue coz aliwaongoza kutoka nje ya Bunge na kutokumtambua JK kama raisi halali wa Tz. Wadau mna mawazo gani kuhusu hili jambo? Kuna uhalali wa Mbowe kufanya alichofanya? Haya ni mawazo binafsi hayana chuki na Mbowe ila nasikitika kuwa viongozi wengine wa Chadema kama wao wataendelea na msimamo wao ili hali Mwenyekiti wao ameshauvunja. Nakaribisha majadiliano Wadau.
 
Ndiyo ukomavu wa kisiasa lakini wafanye hivyo kwa misimamo ya chama na si kila mmoja kujipendekeza
inasemekana hayo ni baada ya mazungumzo ya pinda mbowe na rashid othman


mungu ibariki tanzania
 
Si suluhisho la matatizo ya wtz, kukaa kwao pamoja bado haijatushawishi tuamini kwamba matatizo mengi tulionayo wtz yanafikia mwisho.
 
GO9G1385.JPG
 
JK ameonyesha kutojiamini na ushindi wake...kama ni Rais wa kweli angeendelea kukaa maana yeye ndio supreme halafu Mbowe apige magoti!...halafu Rais hashikwi bega kihivyo..
 
Kama sikosei hii ilikuwa ni mwaka 2005 baada ya uchaguzi uliomtangaza jk kuwa mshindi wa nafasi ya urais. Kwa ujumla, Chadema waliridhika na kuridhia matokeo na hapo kwenye picha inaonekana Kamanda Freeman Mbowe
akimpongeza jk bila kinyongo. Sasa kutokana na picha na maelezo haya, tunaweza kujifunza kwamba uchaguzi wa 2005 ulikuwa huru na wa haki na chadema waliridhika nao. Sasa basi, kama chadema ni chama kilekile na Mbowe, Dr. Slaa (PhD) na viongozi wengine ni walewale, kwa nini leo hii wasishikane mikono na jk? Ukweli ni kwamba uchaguzi wa mwaka huu haukuwa wa huru na wa haki.

Pia, picha hii inaonyesha umakini wa chadema katika kuendesha siasa za nchi hii na ni chama chenye msimamo thabiti wa kusimamia maamuzi yake. Hakina substandards katika kufanya mambo yake. Hongera viongozi wa chadema, wananchi tuna imani nanyi.

Du! huu sasa ni ulevi wa mapenzi, tena wa kitoto. Wewe unaambiwa picha hii ilipigwa siku ya sheria tarehe 2 February, 2011, halafu unaleta hoja zenye ulemavu.
 
Usituletee habari za gazeti la MTANZANIA hapa.
1.CDM walk-out ilikuwa ni kushinikiza katiba mpya(katiba mbovu iliibeba CCM)
2.ni NEC tu yenye kumtambua au kutomtambua mshindi (CDM was not changing any thing)
3.Dr Slaa in his facebook ameandika kuwa hana personal problems with JK, ALSO I HOPE CDM hawana personal and only personal problems with JK (like umri,rangi ujeshi,ubagamoyo,marriage status,malezi na makuzi ya Rz 1,dini yake), ugomvi ni kwenye commitment in utekelezaji wa sera

4.CDM waliukataa mchakato mzima ulimrudisha ikulu JK, so it is CDM (wanainchi) against mfumo ambao JK anayaona matatizo yake ila hataki kuyashughulikia.

My take: MBOWE WAS WORKING ON WORDS OF DR.SLAA (no personal probems=kusalimiana hakugombi)
 
Definition ya neno Politics hapa inajitokeza..Siasa haina uhusiano wowote kununiana,
 
kwa kweli Chadema hawana msimamo na wala hawajijui


hapa walituletea Picha ya lipumba akimpongeza JK akaitwa CCM B mamluki na mengineo na wao vidume waliokacha kumtambua na hawataki hata kumsikia akiongea

leo wamefanya wao, imekuwa Demkrasia, hivi demokrasia akifanya chadema tu? lkn wengine ni mamluki?


hawa watu hawana mpya, wameulisha watu Arusha kwa lipi? wakati leo kila kitu walichopambana nacho kumbe ni uongo tu
 
Back
Top Bottom