Ni miezi kadhaa imepita tangu CHADEMA wakatae kumtambua JK kama raisi halali wa Tz, leo tunaambiwa kwamba mwnkt wa chadema Freeman Mbowe kamtambua JK kama raisi halali wa Tz, najiuliza ni kipi kimefanyika kudhibitisha uhalali wa huyu Mheshimiwa na wakamtambua? Kwangu mimi huu ni undumilakuwili na ukengeukaji! Haiwezekani ukawa mtu kigeugeu namna hiyo. Bwana Mbowe itabidi awashawishi wenzake nao wamtambue coz aliwaongoza kutoka nje ya Bunge na kutokumtambua JK kama raisi halali wa Tz. Wadau mna mawazo gani kuhusu hili jambo? Kuna uhalali wa Mbowe kufanya alichofanya? Haya ni mawazo binafsi hayana chuki na Mbowe ila nasikitika kuwa viongozi wengine wa Chadema kama wao wataendelea na msimamo wao ili hali Mwenyekiti wao ameshauvunja. Nakaribisha majadiliano Wadau.